25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi waaswa kuzingatia taarifa ya hali ya hewa

 Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam



Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, amewataka wananchi kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) kwa sababu taarufa zao kwa asilimia 80 ni za kweli na kwamba zimefanyiwa kazi kwa uhakika.

Akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa awamu ya pili wa taarifa za Hali ya Hewa Kidunia, Profesa Kamuzora amesema taarifa hizo zimekuwa zikiandaliwa kwa ubora ili wananchi waweze kuzitumia.

“Sayansi inayotumiwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), katika utabiri wa hali ya hewa ni ya hali ya juu na kwamba inatoa fursa kwa wananchi kujipanga ili kujiepusha na majanga,” amesema Kamuzora.

Amesema asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima na wachache ni wafugaji hivyo basi wanahitaji taarifa za hali ya hewa ili waweze kupanga ratiba za shughuli zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TMA, Dk Agnes Kijazi, amesema wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari pindi wanapopata taarifa za hali ya hewa na kwamba hali hiyo inaweza kupunguza majanga yatokanayo na hali ya hewa pale wanaposikia Luna mvua kubwa au mafuriko.

“Mkakati wetu ni kuendelea kutoa taarifa sahihi za hali ya hewa ili wananchi waweze kujipanga na kuzifanyia kazi,” amesema Dk. Kijazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles