24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanajeshi, polisi kusimamia zoezi udhibiti Ebola Congo

KINSHASHA, CONGO

MAOFISA nchini Congo wamesema wanajeshi na polisi nchini humo watasimamia zoezi la watu kuosha mikono yao na kupima dalili za homa, baada ya mlipuko wa homa kali ya Ebola kutangazwa kuwa suala la afya la dharura la kimataifa.

Mratibu wa kitengo cha kusimamia juhudi za kupambana na mripuko wa ugonjwa huo katika wizara ya Afya ya Congo alisema jana kuwa wanajeshi na polisi watawalazimisha watu watakaokaidi kuchukua hatua muhimu za kusaidia kuudhibiti ugonjwa huo hatari.

Juzi Shirika la Afya duniani (WHO) lilitangaza hali ya dharura  na inayopaswa sasa kutupiwa jicho na mataifa baada ya maambuki ya ugonjwa wa Ebola kuendelea kusambaa nchini Congo.

Hatua hiyo walisema inaweza kuzihamasisha nchi wafadhili kutoa fedha zaidi.

Pamoja na kutangaza hali ya dharura, WHO haijasema  mipaka ifungwe kwa sababu hatari ya ugonjwa huo  kusambaa nje ya Congo si kubwa.

Mlipuko wa ugonjwa huo umeamua zaidi ya watu 1,600 nchini Congo.

Wiki hii, kesi ya kwanza iliripotiwa katika mji wa Goma wenye watu zaidi ya milioni moja ulio karibu na nchi ya Rwanda.

Kabla ya hapo takribani mwezi mmoja uliopita viliripotiwa vifo vya watu wawili nchini Uganda.

Watu hao, ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano na bibi yake ambao walikuwa wametokea nchini Congo.

Hali kadhalika kulikuwa na hisia za mtu mwingine kupata maambukizi ya ugonjwa huo nchini Kenya lakini baada ya vipimo na matibabu ilionekana yupo sawasawa

Kwa mujibu wa taratibu za kutangaza hali ya dharura (PHEIC), hatua hiyo ni ngazi ya juu ya WHO na imesikika au kutumika mara nne hapo awali.

Hii ni pamoja na ugonjwa huo ulipoenea sana Afrika Magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016, na kuua watu zaidi ya 11,000 .

“Ni wakati wa dunia kuwa makini,” Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika mapema wiki hii mjini Geneva ambapo pia hali ya dharura ilitangazwa.

Alisema amekubali mapendekezo kwamba kusiwe na vikwazo kwa wasafiri au vya kibiashara, au uchunguzi wa kuingilia abiria kwenye bandari na viwanja wa ndege nje ya eneo lililo karibu na zilikoripotiwa kesi za ugonjwa huo.

Alisisitiza kuwa kufunga mipaka kutasababisha janga kwa maisha na ustawi wa watu wanaovuka mipaka kila siku kwa ajili ya biashara, elimu ama kutembelea ndugu zao.

Tayari masharika kama yale ya Msalaba mwekundu na  Red Crescent Societies yameunga mkono hatua  hiyo ya WHO.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles