27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaharakati unyanyasaji wa kingono watunukiwa Tuzo ya Amani Nobel

 Oslo, Norway

Daktari raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Dennis Mukwege, na mwanaharakati kutoka jamii ya Wayazidi nchini Syria, Nadia Murad, wametunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2018 kwa jitihada zao  juu ya kupambana na unyanyasaji wa kingono.

Tangazo la ushindi wa Mukwege na Murad, la Tuzo ya Nobel limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hiyo Berit Reiss-Andersen, mjini Oslo, muda mchache uliopita.

Reiss Andersen amesema, wawili hao wamekuwa viongozi wa mapambano dhidi ya janga la unyanyasaji wa kingono, ambalo limeenea kutoka eneo mmoja hadi jingine, kama vuguvugu za MeeToo zilivyodhihirisha.

“Washindi hawa wawili wametoa mchango mkubwa katika kuumulika na kuupinga uhalifu huo wa kivita. Dennis Mukwege, ni mtu aliyejitolea maisha yake kuwasaidia wahanga hao. Nadia Murad, ni shahidi anayesimulia unyanyasaji, uliofanywa dhidi yake na dhidi ya wengine,” amesema Reiss-Andersen.

Nadia Murad ni mmoja wa wasichana na wanawake wa kiyazidi wanaokadiriwa kufika 3,000, ambao walibakwa na kufanyiwa unyanyasaji wa kila aina na wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, na amejitokeza kwa ujasiri kuzungumzia madhila yaliyomkuta pamoja na wenzake.

Washindi waliotangazwa leo wamechaguliwa kutoka kwenye orodha ya watu 216 na mashirika 115, ambayo ilikuwa imewasilishwa mbele ya kamati. Orodha hiyo ni ya pili kwa ukubwa kuwahi kupokewa na kamati hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles