27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wagoma wakidai kudhalilishwa kingono na walimu, polisi wawatawanya kwa mabomu

Safina Sarwatt, Moshi

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wanafunzi wa shule ya sekondari Majengo baada ya kugoma kuingia madarasani kwa kile walichodai ni kudhalilishwa kingono na kuchaniwa nguo na walimu wao.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya wanafunzi hao kugoma kuingia darasani, kukataa kula chakula na kukusanyika mbele ya ofisi ya Mkuu wa shule hiyo huku wakitaka uongozi wa shule kufanya utatuzi wa sakata hilo.

Wakizungumza na Mtanzania Digital leo Ijumaa Februari 8, baadhi ya wanafunzi hao wamesema wamechoshwa na vitendo hivyo vya kikatili na udhalilishwaji wa kingono huko wakilitaka jimbo Katoliki la Moshi na Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako kuingilia kati.

Kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo Gasto Lucas, amesema kuwa vitendo hivyo wanavyofanyiwa ni vya kudhalilisha utu wao kinyume na taratibu za nchi na wanapoulizia inakuwaje vitendo hivyo vinafanyika wanapigwa.

Kwa upande wake mwanafunzi Anithe Asenga amesema  walimu wamekuwa wakiwanyanyasa wanafunzi wa kike na kuwadhalilisha huku wakichawachania sketi zao mbele  na sehemu za kwenye mapaja.

“Tangu tumefungua shule hii ni sketi ya tatu nachaniwa tu jamani na sketi nimeshoneshewa hapa hapa shuleni nimelipia sh.20000 kwa kila sketi, “amesema.

Aidha akizungumza kwa niaba ya  uongozi wa shule ya sekondari Majengo Mwalimu Mukindia Stephen amesema  kuandamana siyo suluhisho hivyo aliwataka wanafunzi hao watawanyike warudi majumbani na uongozi wa shule utakaa na  uongozi wa serikali ya wanafunzi kuzungumzia suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles