24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wa kigeni marufuku kufanya kazi Uingereza

WANAFUNZI

LONDON, UINGEREZA

WANAFUNZI wa kigeni watapigwa marufuku kufanya kazi wakati wakiendelea na masomo nchini hapa, na watalazimishwa kuondoka mara baada ya kuhitimu.

Sheria hizo mpya zinatarajia kujadiliwa bungeni baadaye wiki hii, baada ya kuwasilishwa wiki iliyopita na Waziri Mkuu mpya, Theresa May wakati alipokuwa bado Waziri wa Mambo ya Ndani.

Serikali imedai kwamba hatua hiyo ikipitishwa na Bunge itasaidia kupambana na udanganyifu kuhusu viza nchini Uingereza.

Sheria hizo zitawahusu tu wanafunzi wasiotoka ndani ya Umoja wa Ulaya (EU), ambao walikuwa sehemu ya wahamiaji 121,000 mwaka jana.

Wanafunzi 51,000 tu wa kigeni waliondoka Uingereza na kuacha kundi kubwa la wanafunzi 70,000 likiendelea kuwa hapa.

May aligusia takwimu hizo ili kutetea harakati zake za kutengeneza sheria kali.

Ana matumaini ya kuzuia wahamiaji kutumia vyuo kama mlango wa nyuma wa kujipatia kirahisi viza za Uingereza, na amepiga marufuku vyuo 870 kupokea wanafunzi wa kigeni.

Hata hivyo, wanataaluma wamekosoa mpango huo dhidi ya wanafunzi wa kigeni wanaokaa Uingereza, wakisema utailetea Uingereza uhaba wa fedha na vipaji.

Professa Paul Webley, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Soas alisema: “Wanafunzi wa kimataifa huleta fedha na iwapo wanabaki, vipaji vyao vinainufaisha Uingereza.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles