27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI 728 WASOMEA CHINI YA MTI WA MWEMBE

Na MWANDISHI WETU,

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Kasindaga Kata ya Kyebitembe wilayani Muleba, wanasomea chini ya mti wa mwembe kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Dauson Rugakingira  alisema wanafunzi hao wanateseka kupata elimu.

Alisema wakati wa mvua   ufundishaji husimama kwa kuwa chini ya mwembe huvuja.

Alisema shule hiyo ina wanafunzi 728 na vyumba vitano vya kusomea darasa la awali hadi la tatu na darasa la saba madarasa mengine wakisomea chini ya mwembe hivyo ina mahitaji vyumba vya madarasa 16.

“Wakati mwingine tunalazimika wanafunzi wa darasa la nne na la tano pia darasa la sita na saba kuwaunganisha kuwa darasa mseto na kuwafundisha mada zinazorandana katika ufundishaji   kuokoa muda,” alisema Rugakingira.

Alisema shule hiyo yenye walimu saba haina nyumba ya walimu hata moja na walimu wa shule hiyo wanaishi kwenye makazi ya wananchi kwa kukodi.

Rugakingira alisema  walimu wengine kutembela umbali mrefu kutoka vijijini na wengine hupata ajali za pikipiki wanapokuwa wakitoka shuleni ama nyumbani na kudhoofika katika utendaji

Naye Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nshanje Joseph Sanga,   alisema wanafunzi wa shule hiyo nao wamekuwa wakisomea chini ya miti kutokana kuwa na vyumba vitatu kati ya vyumba 10 vya madarasa na wanafunzi 430.

Alisema kwa kuwa  shule hiyo iko jirani na barabara kuu imekuwa ikisababisha kelele na hivyo kukosa usikivu wakati wa kujifunza hivyo kuwakwamisha kimasomo.

Sanga alisema   shule hiyo inatumia vyumba vitatu kati ya vyumba 10 vya madarasa na nyumba za walimu miaka 10 ikiwa na wanafunzi 430.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles