31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 44 Kenya wajiunga makundi ya kigaidi

Profesa David Some
Profesa David Some

NAIROBI, KENYA

WANAFUNZI zaidi ya 44 kutoka vyuo vya elimu ya juu vya umma na binafsi wamejiunga na makundi ya kigaidi yanayopigana nchini Somalia na Libya, Tume ya Taifa ya Elimu ya Juu Kenya (CUE) imesema.

Afisa Mkuu Mtendaji wa CUE, Profesa David Some aliliambia kongamano la vyuo vikuu lililomalizika Alhamisi jioni ya wiki iliyopita kuwa miongoni mwao, 17  ni wasichana.

Profesa Some alihimiza makamu wakuu wa vyuo kuwa macho akisema makundi ya kigaidi yanawalenga wanafunzi wa elimu ya juu ili kutumia werevu wao kutekeleza maovu.

“Makundi ya kigaidi yanalenga wanafunzi wanaosomea udaktari, uhandisi, uanasheria, uuguzi na saikolojia miongoni mwa mafunzo mengine,” alisema katika katika kongamano hilo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, mjini Nairobi.

Kozi hizo zinafuatiliwa zaidi na makundi ya kigaidi kwa vile yanajipatia wauguzi na madaktari wa kuwatibu, mawakili wa utetezi na wahandisi wa kuunda silaha.

Profesa Some aliwataka makamu wakuu wa vyuo kufanya lolote lile kuzuia magaidi kusajili wanafunzi wao akisema suala la ukosefu wa usalama katika vyuo vikuu linapaswa kuchukuliwa kwa uzito zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles