25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 300 wapata ujauzito Mwanza, waruka ukuta usiku kutafuta wanaume uraiani

BENJAMIN MASESE- MWANZA

Ripoti ya  sekta ya elimu kwa Mkoa wa Mwanza imeonyesha  kuwa mwaka 2018  jumla ya wanafunzi 300 wa  shule za  msingi na Sekondari walipata ujauzito huku kesi nyingi zikionekana kuishia vituo vya polisi na ofisi za kata.

Pia ripoti hiyo imebainisha kwamba baadhi ya wanafunzi wanaoishi shule za bweni wamekuwa na tabia ya kutoroka usiku na kuwafuata wanaume uraiani ambapo baadhi yao wamekutawa na simu zinatumika katika mawasiliano ya mapenzi.

Akiwasilisha ripoti hiyo juzi katika  kikao cha semina ya  iliyohusishana kamati ya  mkoa  ya ulinzi wa wanawake na watoto na Shirika  la la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini), Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mwanza, Jovitha Mwombeki alisema ripoti hiyo ni ya  halmashauri nane za mkoa huo.

Alifafanua kuwa  kwa upande wa shule za msingi, wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni ni 49 ambapo Ilemela zilikuwa mbili, Kwimba 11, Magu 26, Jiji la Mwanza 3, Sengerema 9, Ukerewe 9, Buchosa na Misungwi hakiwa na matukio hayo.

Mwombeki alisema upande wa Sekondari mimba zilikuwa 251 ambapo Buchosa 23, Ilemela 2, Kwimba 42, Magu 17, Misungwi 98, Jiji la Mwanza, 36, Ukerewe 32 huku Sengerema haikupata tukio la mimba.

“Katika  kukabiliana na suala hili la ujauzito kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa walioshiriki kuwapatia mimba hawa watoto wetu, mfano Buchosa kuna matukio 23 ya msingi na sekondari  ambapo kesi zote zipo polisi, Ilemela kuna mimba tano na kesi zote zipo polisi.

“Kwimba kuna  mimba 53 ambapo  kesi 37 zipo polisi, 10 zipo mahakamani na sita zipo kwa watendaji wa kata  wakiendelea kuchunguza  na kuwatafuta watuhumiwa, upande wa Magu jumla ya  mimba 43  na zote zipo kwa watendaji wa kata, Misungwi ni mimba 98 na kati ya hizo 54 zipo polisi, 37 mahakamani na tano zimehukumiwa.

“Mwanza jiji kuna jumla ya mimba 39  na zote zipo kwa watendaji wa kata  wakiwatafuta watuhumiwa, Sengerema kesi za mimba zipo tisa ambapo zote zipo polisi na Wilaya ya Ukerewe mimba ni 41 na zote zipo polisi,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles