31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 1,000 wakimbia mtihani wa ‘mock’ Mwanza

BENJAMIN MASESE -MWANZA

SERIKALI mkoani Mwanza imelazimika  kuwakutanisha maofisa elimu wilaya, kata na wakuu wa shule kufanya tathmini ya mitihani ya darasa la saba na kubaini baadhi ya changamoto zilizofanya wanafunzi 1,034 kutofanya mtihani wa majaribio ‘mock’.

Pia kikao hicho kimekusudia kupata majibu kutoka kwa maofisa hao kueleza sababu ya baadhi ya halmashauri kutofikia asilimia 90 ya ufaulu ambao ni lengo la mkoa huo.

Kwa mujibu wa takwimu za mkoa, Halmashauri ya Ilemela ilifikia asilimia 98.3,  Sengerema 97.1,  Misungwi 96.6, Jiji la Mwanza 95.2, Magu 92, Ukerewe 85.4, Kwimba 84.6 na Buchosa 80.5.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana baada ya kufungua kikao na maofisa hao, Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Michael Ligola, alisema lengo ni kuweka mikakati na kutatua changamoto  zilizopo ili kila halmashauri iweze kufikia  asilimia 90 ya ufaulu katika mitihani ya kitaifa.

Alisema katika mitihani  ya majaribio iliyofanyika ngazi ya mkoa, baadhi ya halmashauri   ziliweza kufikia asilimia 90, lakini nyingine asilimia 80, hivyo kitendo cha kuwakutanisha maofisa elimu  ni kutaka kuwa kwenye  mstari unaofanana.

Ligola alisema wanafunzi 1,034 ambao hawakufanya mtihani huo, kati yao wavulana ni 347 na wasichana 687 sawa na asilimia 1.5, hivyo alisema kiwango hicho ni kikubwa na kinapaswa kutafutiwa suluhisho.

“Bila shaka kila mmoja atasema na baadaye tutajadiliana kuona wapi panatakiwa kurekebishwa ili mtihani ujao tuweze kufanya vizuri.

“Kwa habati nzuri Mkoa wa Mwanza hali ya taaluma si mbaya, hivyo matarajio yetu shule zilizofaya vibaya tutasikia sababu zao ni zipi na tutaelezwa wale waliofanya vizuri wao walifanya nini,” alisema.

Ofisa Elimu Kata ya Nyamanoro, Iloze Ngereza, alisema licha ya eneo lake kufanya vizuri katika mitihani ya majaribio, changamoto kubwa iliyopo ni utoro wa wanafunzi.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bujingwa, Wilaya ya Kwimba, Mathias Tito, alisema shule yake ni miongoni kwa shule zilizofanya vibaya, hivyo kikao hicho kitasaidia kubadilishana mbinu zitakazofanya halmashauri zote kuwa katika mstari mmoja.

mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles