31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WANACHAMA CCM WATAKIWA KUBADILIKA KIFIKRA

flyvria5

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, kimewataka wanachama wake kubadilika kifikra ili kuendana na muundo mpya wa chama hicho.

Hivi karibuni kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), chini ya Mwenyekiti wake Taifa, Rais Dk. John Magufuli, kilibariki mabadiliko makubwa ya muundo wa chama kwa kupunguza idadi ya vikao na wajumbe wa ngazi zote.

Akizungumza jana wakati wa kuwapokea wanachama wapya katika Tawi la Kimanga Kuu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, alisema mabadiliko hayo yataleta mageuzi makubwa ndani ya chama hicho.

Wanachama hao ambao wamehama kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ni Mwalimu Anthony Gella, Joel Sasabo, Daniel Ndengetu, Samuel Lyimo na Joseph Chausi.

“Mabadiliko haya yanatuhitaji na sisi tubadilike kifikra, tusiendelee kuwa ving’ang’anizi wa madaraka, ukiona umetimiza wajibu wako na unaona kuna mwenzako anafaa mpishe,” alisema Madabida.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assah Simba, alisema Kata ya Kimanga licha ya kusumbuliwa na upinzani pia ilikuwa inaongoza kwa kuwa na migogoro ya ndani.

“Lazima tuambizane ukweli Kimanga mlikuwa mnaongoza kwa migogoro ya ndani na sasa hivi chama chetu kinarudi kwenye mstari ndio maana mnaona wenzetu wanaanza kurudi, hivyo muwapokee na kukaa nao vizuri waone tofauti na kule walikokuwa,” alisema Simba.

Awali Mwalimu Gella ambaye alikuwa Katibu wa Kata ya Kimanga, alisema amehama Chadema kutokana na kukerwa na tabia ya viongozi wa wilaya na mkoa aliodai kuwa ni wababe, wabaguzi na kwamba wanaikanyaga katiba.

Kwa upande wake Sasabo ambaye alikuwa Katibu wa Baraza la Wazee Jimbo la Segerea, alisema anarudi CCM baada ya kuona hivi sasa kuna mwanga kwani mambo mengi waliyokuwa wakiyapigania Rais Magufuli anayatekeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles