25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wamiliki shule binafsi wafukuzana

Na Samwel Mwanga, Dar es Salaam

UMOJA wa Wamiliki na Mameneja wa Taasisi Binafsi za Elimu Tanzania (Tamongsco) umetangaza kumfukuza kazi Katibu Mkuu wake Benjamin Nkoya akidaiwa kukosa sifa ya kushika wadhifa huo.

Kwa mujibu wa barua ya Oktoba 20, mwaka huu iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Tamongsco Kanda ya Dar es Salaam, Kachwamba Aboubakar, licha ya Nkoya kuwa kiongozi wa taasisi hiyo kwa muda mrefu, lakini hajawahi kulipa ada ya uanachama kwa miaka mitano kinyume cha katiba yao ibara ya 18.1(c).

“Baada ya kugundua tatizo hilo, ofisi ya Katibu wa Kanda iliamua kutembelea shule ya Nkoya iitwayo Golden Rule kule Tuangoma. Ofisi ilipofika katika eneo la shule ilimshirikisha Mratibu Elimu Kata ya Tuangoma, aliwapeleka wajumbe hadi mahali ilipo shule ya Golden Rule, walishuhudia na kuthibitisha kuwa shule hiyo imesimama kwa muda mrefu kwani majengo yamezingirwa na pori la nyasi na hakuna dalili ya wanafunzi au watu wanaoishi katika eneo hilo,” ilisema sehemu ya barua
hiyo iliyotumwa kwa mwenyekiti wa umoja huo taifa, ambayo MTANZANIA imeona nakala yake.
Barua hiyo ilieleza kuwa hata majirani wa shule hiyo wamethibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa shule hiyo ilishajifunga kwa zaidi ya miaka mitano kwa kukosa wanafunzi, hivyo ofisi ya kanda kuamua kuandika barua rasmi kuwa Nkoya amekosa sifa ya kuendelea kuwa mwanachama katika kanda hiyo.

Nkoya alipoulizwa kwa simu juu ya suala hilo, alidai kuwa hawezi kuondolewa kwenye nafasi hiyo na kikao cha kanda isipokuwa Kamati Kuu ya umoja huo ambayo wajumbe wake ni wenyeviti na makatibu wakuu wa kanda zote.

“Mimi ni Katibu Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam hadi Februari mwakani,” alisema Nkoya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles