33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WALIOKUMBWA NA MAFURIKO LONGIDO WAPATIWA MTUMBWI

Na Janeth Mushi, Longido


Kijiji cha Leremeta kilichopo Kata ya Sinya wilayani hapa, kilichozingirwa na maji kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, wamekabidhiwa msaada wa mitumbwi miwili kwa ajili ya kusafirisha vyakula wagonjwa na wanafunzi.

Mitumbwi hiyo ilikabidhiwa leo Jumapili Machi 25, na Mbunge wa Jimbo la Longido, Dk. Steven Kiruswa (CCM), kwa uongozi wa kijiji hicho ili kuwasaidia wananchi hao kupata muhimu ikiwamo chakula na afya.

Dk. Kiruswa alisema baada ya tathmini waliyofanya bila mitumbwi au helikopta ya kupeleka huduma kwa wananachi, kaya 255 zilizopo kijijini hapo ziko hatarini kukosa huduma hizo muhimu.

Amesema mitumbwi hiyo imetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Honey Guide Foundation, mitumbwi ambayo imeanza kutumika kusafirisha misaada ya vyakula inayotolewa na wahisani kwa ajili ya wananchi hao ambao bado wanazungukwa na maji yenye kina kirefu.

“Niwashukuru Honey Guide kwa msaada wa hii mitumbwi hii na kama tulivyoona inaweza kubeba mifuko 20 ya unga kila mtumbwi na vijana watakaa hapa hadi maji yatakapokwisha na wananchi kuweza kupata huduma mbalimbali na kwa kuwa hii ni kata ya pembezoni na tulishajenga shule ya bweni hapa katika kijiji cha Oldonyo na tukahimiza wapeleke watoto shule ya bweni, shule zitakapofungwa watasafirishwa na mitumbwi hii.

“Natoa wito kwa wananchi endapo maji hayo yatapungua, wafunge maboma yao na kuhamia vijiji vya jirani vyenye huduma zote muhimu ili waweze kupata mahitaji yao ya kila siku na kuondokana na adha hiyo wanayokabiliana nayo kwa sasa,” amesema.

Naye Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Seremon Laizer amesema wameweka utaratibu na usimamizi wa kuhakikisha vyakula hivyo vya msaada vinawafikia walengwa hadi maji hayo yatakapopungua na wananchi hao kuweza kuendelea na shughuli zao kama kawaida ambapo hadi sasa wameshapata unga wa dona zaidi ya tani moja zilizotolewa na watu mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles