33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waliokatwa majina Serikali za Mitaa watua CCM Dar

CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

WANACHAMA wa CCM walioomba na kudai kushinda kura za maoni kuwania kugombea uenyekiti wa mtaa na ujumbe, wamefika ofisi za chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam kupinga kukatwa majina yao na Halmashauri Kuu za Wilaya ambazo ndio hufanya uteuzi wa mwisho.

Kwa upande wake, chama hicho kimesema kuwa kamwe hakitaweza kumpitisha mgombea yeyote katika nafasi ya Serikali za Mitaa endapo ana kasoro zilizoainishwa na kukatazwa kwa mujibu wa kanuni za chama hicho.

Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu uteuzi wa wagombea wao, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Zakaria Mwansasu, alisema hata kama mgombea ameshinda kura za maoni, wapo tayari kumwacha na kumpa nafasi hiyo mgombea aliyeshika nafasi ya pili.

Alisema kanuni za CCM zinazoongoza jinsi ya kuwapata wagombea hao zipo wazi, hivyo kwa mgombea yeyote anayeona ameonewa ni vyema akaleta malalamiko yake ndani ya chama.

“Hatupo tayari kumteua mgombea ambaye aliwahi kupatikana na kesi ya jinai, au aliwahi kufanya ubadhirifu wa aina yeyote ndani ya mtaa au nje ya eneo lake, hatutampa nafasi, atakuwa amepoteza sifa,” alisema Mwansasu.

Aliongeza kuwa chama hicho kipo imara na wapo tayari kuwashughulikia wote watakaokiuka kanuni na taratibu za uchaguzi.

“Tumewapa mafunzo wanachama wetu wameiva, hivyo kila anayeonekana kukiuka wamekuwa wakitoa taarifa ofisini na sisi tunazifanyia kazi haraka iwekezenavyo,” alisema Mwansasu.

Mwansasu alisema ni lazima wagombea watambue kwamba kuongoza kura za maoni si ushindi kwakuwa ikithibitika umetumia njia ambayo si sahihi uteuzi huo utatenguliwa.

“Wapo wengine waligombea kinyume na taratibu, mfano makatibu waenezi, wenyeviti wa vijana, hao wote wametenguliwa kwa kuwa hawakutakiwa kugombea,” alisema Mwansasu.

Alisema awali walipokea malalamiko kwenye baadhi ya kata na mitaa kuhusu uteuzi wa wagombea hao na waliagiza uchaguzi urudiwe na tayari kumefanyika marudio.

“Katika marudio hayo, wapo ambao walishindwa lakini hawakuwa na sifa, hivyo tumeamua kuwaweka pembeni na mchakato wa uchaguzi huo unaendelea, ikiwamo uchukuaji wa fomu,” alisema Mwansasu.

MTANZANIA lilishuhudia baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiwa wamefurika ofisi za Katibu Mwansasu kulalamika jinsi mchakato ulivyokwenda katika mitaa yao na walikabidhi barua za malalamiko.

Miongoni mwa mitaa ambayo inadaiwa wagombea wao wamebadilishiwa matokeo, ni pamoja na Mtaa wa Mongo la Ndege, ambako aliyekuwa akiitetea nafasi yake, Rajab Tego, alidai kuwa ameshinda kura za maoni kwa kupata 230 lakini aliyetangazwa mshindi ni mgombea aliyemfuata.

Mtaa mwingine ni Muungano Kata ya Goba, ambako mgombea aliyeshinda Lazaro Sentimoja aliitwa ofisi za kata na kunyang’anywa ushindi wake bila kuelezwa sababu za kufanya hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles