30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Walioingia na kutoka usajili wa VPL 2016/17

Laudit Mavugo
Laudit Mavugo

NA ZAINAB IDDY,

LIGI Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbalimbali vya Tanzania Bara.

Kabla ya Ligi hiyo kuanza, kutakuwa na mechi ya Ngao ya Hisani inayoashiria kufunguliwa kwa mtanange huo msimu wa 2016/17 kwa kuwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga SC dhidi ya Azam FC.

Kuelekea msimu mpya wa ligi tumeona timu zote 16 zikijiandaa vilivyo kuhakikisha zinaleta ushindani, miongoni mwa mambo waliyoyafanya ni usajili wa wachezaji wapya kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi.

Mbali na kusajili, pia katika kipindi hicho timu mbalimbali ziliweza kuweka wazi juu ya wale waliowaacha kutokana na sababu mbalimbali.

SPOTIKIKI leo inakuletea sajili za timu zinazoshiriki Ligi Kuu msimu wa 2016/17 na wachezaji walioachwa, lengo ni kukufahamisha mchezaji gani ataonekana kwenye timu ipi msimu ujao.

Azam FC

Msimu huu Azam FC itakuwa chini ya benchi la ufundi la Wahispania likiongozwa na kocha Zeben Hernandez, aliyechukua mikoba ya Stewart Hall ambaye alijiuzulu mara baada ya kumalizika kwa Ligi msimu uliopita.

Msimu huu Azam haijaongeza mchezaji wa ndani na badala yake imewapa mikataba wachezaji wa kigeni ambao ni mabeki Bruce Kangwa anayetokea Highlanders ya Zimbabwe, Daniel Amoah na winga Enock Agyei kutoka Medeama ya Ghana, huku wakiwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji waliomaliza kandarasi zao akiwemo Frank Domayo na kuwapandisha Ismail Gambo, Idi Shaaban na Abdalah Msoud .

Waliotolewa kwa mkopo

Beki Abdallah Kheri amepelekwa Ndanda FC na kiungo Bryson Raphael, winga Joseph Kimwaga amejiunga Mwadui pamoja na washambuliaji Kelvin Friday aliyerejea Mtibwa Sugar na Ame Ally ‘Zungu’, aliyekwenda Simba, huku ikiachana na Ivo Mapunda, Didier Kavumbagu, Allan Wanga, Racine Diof na Said Morodi na Kipre Tchetche wakati Farid Mussa akipelekwa klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania kwa makubaliano maalumu.

Yanga SC

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu chini ya kocha wao, Hans van der Pluijm ambaye ndiye aliibuka kocha bora msimu uliopita, katika kuimarisha kikosi chao wameweza kuwasajili Beno Kakolanya(Tanzania Prisons), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Hassan Kessy (Simba), Obrey Chirwa (FC Platinum, Zimbabwe) na Juma Mahadhi (Coastal Union), huku wakiwaacha Salumu Telela, Poul Nonga, Issofou Boubakari na Benedict Tinoko.

Simba SC

Msimu mpya wapo chini ya kocha Joseph Omog, aliyewahi kuinoa Azam FC na kuipa ubingwa, huku kocha Jackson Mayanja aliyemaliza nayo ligi akiwa msaidizi wa benchi la ufundi.

Katika kuhakikisha kikosi cha Wanamsimbazi kinakuwa moto, kimewaongeza Ame Ally (Azam FC), Maliki Ndeule, Jamli Mnyate na Emannuel Semwanza  (Mwadui FC), Hamad Juma (Coastal Union), Besala Bokungu na Fuad Mussa (Congo), Method Mwanjali (Zimbabwe), Laudit Mavugo (Vital O), Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Mudhamir Yasin (Mtibwa Sugar).

Hassan Kessy, Hassan Isihaka na Peter Mwalyanzi wametolewa kwa mkopo, Justice Majabvi, Brian Majwega, Raphael Kiongera na Hamisa Kiiza.

Mtibwa Sugar

Mtibwa msimu huu itakuwa chini ya kocha Salum Mayanga aliyechukua mikoba ya Meck Mexime.

Kuelekea Ligi hiyo Mtibwa imewasajili wachezaji Rashid Mandawa (Mwadui FC), Cassian Ponera (Ndanda FC), Haruna Chanongo (Stand United) na Benedict Tinoco kutoka Yanga.

Walioondoka ni Andrew Vicent, Mudathir Yahaya, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahimu na Hussen Sharifu  ‘Cassilas’.

Mbeya City

Kikosi hicho kinachoingia msimu wa nne katika Ligi hiyo, kinaendelea kunolewa na kocha Mmalawi Kinnah Phiri, aliyerithi mikoba ya Meja Mstaafu Abdull Migange.

Mbeya City ilionekana kuwa tishio katika msimu wake wa kwanza kwenye ligi ilipokuwa na kocha Juma Mwambusi.

Kikosi hicho kimewaongeza Rajab Zahir (Stand United), Ayoub Semtawa na Fikiri Bakari (Coastal Union), Owen Chaima na Sankani Mkandawile (Big Bullets, Malawi), Murutabose Mohamed (Timu ya taifa ya Burundi), Isihaka Rajab na Yahya Omari (Africans Sports), Mohamed Mkopi (Tanzania Prisons) na Mark Makolo (Azam FC).

Waliowaacha

Haningtony Kalyesubulu, Yusuph Abdallah, Deo Julius, Hamad Kipopa, Yohana Morris, Richard Peter, Richard Chundu na mshambuliaji  Themi Felix.

Kagera Sugar

Msimu mpya wa ligi watakuwa chini ya kocha Meck Mexime, aliyetokea Mtibwa Sugar ambayo amedumu nayo kwa takribani miaka mitano iliyopita.

Chini ya kocha huyo imeweza kuwasajili wanandinga Hussen Sharif ‘Casillas’ (Mtibwa), Hassan Khatibu na Edward Christopher (Toto Africans), David Burhani, Godfrey Taita na Danny Mrwanda (Majimaji FC), Ibrahim Twaha (Coastal Union).

Walioachwa

Adam Kingwande, Ibrahim Job na  Salum Kanoni, pia imewaongeza mikataba mipya na kuwapandisha wachezaji wa timu yao ya vijana.

Mwadui FC

Imepanda Ligi Kuu ikiwa chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na ndiye atakayeendelea kuinoa kwenye ligi msimu unaokuja.

Kikosi hicho cha Wachimba madini kimefanikiwa kuwasajili Salum Kanoni (Kagera), Nassoro Masoud ‘Chollo’(Stand United), Abdallah Seseme, Athuman Madenge, Miraji Athuman(Toto Africans), Willium Lucian ‘Gallas’ (Ndanda FC), Pastory  Athanas (Stand United), Geofrey Wambura (Coastal Union) na Poul Nonga (Yanga).

Huku walioachwa ni Nizar Khalfani, Razack Khalfani, Kelvin Sabato, Athuma Idd ‘Chuji’, Jabir Azizi, Emannuel Semwanza, Jamal Mnyate na Mlaiki Ndeule.

JKT Ruvu

Msimu mpya wa ligi watakuwa chini ya kocha Malale Hamsini aliyeyetokea Zanzibar, lakini aliweza kuinusuru Ndanda isishuke daraja msimu uliopita.

Malale ameingia kwa maafande hao kuvaa viatu vya  Abdallah Kibadeni, aliyepewa majukumu  mapya kwenye timu hiyo ya kuwa mshauri wa benchi la ufundi.

Kikosi hicho ambacho msimu uliopita kiliponea chupuchupu kushuka daraja, katika kipindi cha usajili kuelekea msimu ujao kimefanikiwa kuwasajili Atupele Green (Ndanda FC), Rahim Juma, Ramadhan Pere na  Hassan Magurumu (Africans Sports), Ismail Amour (JKU) huku ikiwapandisha kutoka kikosi ‘B’, Hamis Ndiyunze, Dickson Choto, Daud Mbaga, Joseph Lunda na Zuber Mlingo.

JKT Ruvu imeachana na wachezaji wake Abdulrhaman Mussa na Gaudiance Mwaikimba.

Ndanda FC

Waliowasajili Abdallah Kheri (Azam FC) na Salumu Telela(Yanga).

Waliowapa mkono wa kwa heri ni Atupele Green, William Lucian ‘Gallas’ na Cassian Ponera,

Stand United

Kikosi hicho kitakachoendelea na kocha Patrick Liewig, kwenye usajili kuelekea msimu ujaa kimeweza kuwasajili, Joseph Owino (URA) na Chidiebere Abasirim (Coastal Union), huku ikiwapa mkono wa kwa heri Haruna Chanongo, Nassoro Masoud ‘Chollo’, Rajab Zahiri, Abuu Ubwa, Hassan Banda,  Phili Methusele na Pastory Athanas.

Majimaji FC

Tangu kuachwa na kocha wake Kally Ongala, aliyemaliza nayo ligi msimu uliopita , imekuwa haina kocha mkuu lakini uongozi umeweza kufanya usajili wa wachezaji kadhaa kulingana na ripoti aliyoiacha Ongala ambao ni Agathon Antony (Kagera), Aman Simba (JKT Oljoro), George Mpole (Kimondo FC), Seleman Kibuta (Mtibwa), Yusuph Mgwao(Friend Ranges), Baraka Mwakakangale (Mwadui FC), Paul John (Polisi Moro), Hamad Kipopile (Mbeya City) na  Dalngithon aliyetokea Nigeria.

Wanandinga walioachana nao ni Godfrey Taita, Danny Mrwanda na David Burhani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles