25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Walioahidi kuchangia ‘Chozi la Fukara’ waingia mitini

Muigizaji JohaNA MANENO SELANYIKA

MWIGIZAJI chipukizi nchini, Martine Tiho, amewataka wabunge, wasanii wenye majina makubwa katika sanaa na watu maarufu walioahidi michango ya fedha wakati alipozindua filamu yake ya ‘Chozi la Fukara’ watekeleze ahadi hizo ili aweze kukamilisha na kuipeleka filamu hiyo sokoni mapema kama alivyopanga.

Tiho alisema hakuna aliyekumbuka kutoa fedha walizomwahidi hivyo ameona bora awakumbushe kupitia gazetini kwamba filamu yake inatakiwa kuwa sokoni mapema mwishoni mwa mwezi huu ikiwa chini ya kampuni ya ‘Boyoge Film’ na usambazaji utafanyika chini ya kampuni ya Mbura Entertainment zote za jijini Dar es Salaam na muda walioahidi kumpa fedha hizo umepita.

“Wakati wa uzinduzi niliwaalika wadau wa filamu kutoka sekta mbalimbali walikuwepo waliokuwa wakigombea ubunge, wabunge, viongozi wengine mbalimbali, wasanii wenye majina makubwa kwenye sanaa mbalimbali na watu maarufu na wengi wao waliofika waliahidi kunipatia fedha baada ya siku kadhaa lakini hadi leo muda mrefu umepita hakuna aliyenipigia simu wala kunipatia kiasi chochote walichoahidi ndiyo maana nawakumbusha kupitia gazeti kwa kuwa wanajijua,” aliongeza Tiho.

Mwigizaji huyo mwenye ulemavu wa mguu pia ni mwimbaji wa muziki wa Bongo Fleva katika filamu hiyo anayotarajia kuiachia mwishoni mwa mwezi huu, ameshiriki kama mshiriki mkuu akiwa na wasanii wengine zaidi ya 10, maudhui ya filamu hiyo yanaelezea jinsi watu wenye ulemavu na umasikini ambapo mikopo imehusika kuongeza umasikini kwa watu wanaoitumia bila kujipanga,” alisema.

Pia inaelezea namna ambavyo wasanii wanadhulumiwa na kudharauliwa katika kazi zao kwa kutokujua haki zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles