24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Walioachiwa sakata dawa za Serikali wakamatwa tena

Mwandishi Wetu- Morogoro

MKUU  wa Mkoa wa Morogoro, Loatha Sanare amegeuka mbogo baada ya kupata taarifa za kuachiwa watu wanaodaiwa kukamatwa na dawa za Serikali kinyume cha sheria kuachiwa.

Kutokana na hali hiyo, aliagizwa kukamatwa mara moja na kurudishwa mahabusi. Sanare aliamua kufanya ziara ya kukagua kituo cha afya na kujiridhisha na taratibu za kupokea dawa.

Katika ziara hiyo,Sanare aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Chonjo, Katibu Tawala wa Mkoa, Mhandisi Emanuel Kolobelo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Morogoro, Rehema Bwasi na Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Robert Manyerere. Baada ya kufika zahanati ya Kinole na kufanya mahojiano na daktari wa zahanati hiyo,Dk. Johnson Nyamuhanga na muuguzi mwandamizi, Mohamed Mbega alionekana kutoridhishwa na majibu.

Katika mahojiano hayo, ilibainika malalamiko ya upotevu wa dawa ni ya muda mrefu ambayo yalisababisha mwenyekiti wa kamati ya zahanati,Moshi kuondolewa madarakani. Pia ilibainika utaratibu wa kupokea dawa ma kutoa haukuwa umekaa sawa, karatasi nyingi za makabidhiano zikiwa hazijatimiza vigezo.

Baaada ya kuona upungufu huo, aliagiza mara moja, Dk. Nyamuhanga Mbega wakamatwe ili wakaunganishwe kuhojiwa na polisi juu ya wizi huu. 

Taarifa zinasema mganga mkuu wa wilaya alipata taarifa ya dawa zilizokutwa kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi, zikiwa na nembo ya Serikali kwa njia ya simu baada ya kupigiwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kinole Februari  29, mwaka huu. 

Alisema Machi 2, mwaka huu timu ya uendeshaji Huduma za Afya ya Wilaya (CHMT), ilikwenda Kinole kwa ufuatiliaji na kubaini suala hilo.

“Baada ya kumwandikia mgonjwa akanunue dawa, ambayo ilikua imeisha kituoni,alienda kununua dawa hizo ambazo zilikuwa na nembo ya Serikali ndipo msako ukaanza kupitia maduka matatu yaliyokuwa ya eneo hilo. Baada ya kukutwa na dawa zenye nembo ya MSD walichukuwa hatua ya kuwakamata na kuwapeleka polisi kituo cha Mkuyuni,”alisema.

Maduka yaliyokutwa na dawa hizo linamilikiwa na Ellenestina Jeremia, muuzaji Zuhura Hamis. Dawa zilizokutwa  ni ALU ya 4 strip 10 = 240 (Ilioana na batch namba ya sales invoice no 6498968 ya zahanati ya Kinole, ALU ya 2 strip 7 =   44 na Cotrimoxazole tabs 22 

Duka la pili, linamilikiwa na Juma Ramadhani na muuzaji Tumie Ally ambako kulikutwa dawa aina ya Depo povera injection 21 vial batch no AG 4104.

Duka la tatu, linakiliwa na Salma Mwambe, muuzaji Grace Edson

 Kulikutwa Depo injection ampule 9 batch no AA 3388,Cannular green Gauge no 18= Moja yenye nembo ya MSD

Lignocane yenye nembo ya serikali (MSD) vial 1 (Mls 50) 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles