27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu wa Hisabati watakiwa kupima wanafunzi wao

LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

WALIMU wa wa somo la hisabati wametakiwa kujenga tabia ya kuwapima wanafunzi kwa kuangalia uwezo wao wa kufikiri na kuelewa mambo badaya ya kuangalia jibu sahihi pekee.

Kauli hiyo ilitolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza, Profesa Theresa Hopfenbeck wakati akiwasilisha utafiti kupima kwa ajili ya kujifuza uliofanyika katika katika warsha iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Aga Khan Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Profesa Theresa alisema utafiti huo ulibuniwa kuelewa namna ya kutumia mbinu za kupima kwa ajili ya kujifunza ambazo zimeshatumika sehemu mbalimbali duniani jinsi zinavyoweza kutumika katika maeneo yenye changamoto hasa katika nchi za bara la Afrika ikiwamo Tanzania.

Alisema kupitia mradi huo ulioanza kutekelezwa nchini mwaka 2016 ukishirikisha walimu 40 kutoka shule sita, umeonesha kuwa na mafanikio makubwa baada ya kuwawezesha walimu kukabiliana na changamoto mbalimbali iliwamo idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa moja.

“Licha ya idadi kubwa ya wanafunzi walimu walionesha uwezo mkubwa wa kuwaweka pamoja wanafunzi katika makundi ili waweze kujifunza, kwa nchi za Ulaya darasa moja ni kati ya wanafunzi 25 hadi 30, lakini katika shule ambazo tumezifikia darasa moja lina wanafunzi 80 hadi 170” alisema Profesa Theresa.

Alishauri walimu na mtandao wa ufundishaji unaohusisha walimu wa somo husika, walimu wakuu na hata kusirikiana na walimu wa shule nyingine ili kuboresha mbinu za ufundishaji.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, Veronica Sarungi, alisema lengo la utafiti huo ni kusaidia wanafunzi kuinua viwango vya ujifinzaji.

“Mbinu ambayo tulikuwa tumeifikiria ilikuwa ni kupitia walimu kwa kuwaongezea umahiri wao katika upimaji katika kufahamu mwanafunzi alipo na namna ya kumsaidia katika ujifunzaji wake.

“Utafiti huu ulikuwa ni wa miaka mitatu ulianza Aprili 2016 na unamalizika Juni mwaka huu na kwa hapa Tanzania ulikuwa umejumuisha baadhi ya shule za Temeke, na tukuwa tumeangalia vigezo kwamba zile ni shule ambazo zina changamoto.

“Tulitewatendelea walimu kuona wanavyofundisha na kuongea nao baada ya kufundisha kuona ni sehemu gani zilikuwa na changamoto. Vilevile utafiti ulifanya majaribio kuangalia maendeleo ya wanafunzi katika hisabati” alisema Anna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles