33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu kusaidia wanafunzi wa kike shuleni

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

Serikali imesema inao utaratibu kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa katika kila shule ya msingi na sekondari wanateuliwa walimu wa kike wa kuwasaidia wanafunzi wa kike hususan katika masuala yanayohusiana na ushauri nasaha.

Hayo yameelezwa leo Mei 31 bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mwita Waitara, wakati akijibu swali la Mbunge wa Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki (CCM).

Katika swali lake, Ndaki alihoji, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi au sekondari kunakuwa na walimu wa kike kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike hasa katika masuala yanayohusiana na hedhi salama.

Akijibu, Naibu Waziri Waitara amesema Serikali inao utaratibu kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa katika kila shule ya msingi na sekondari wanateuliwa walimu wa kike wa kuwasaidia wanafunzi wa kike hususan katika masuala yanayohusiana na ushauri nasaha.

Alisema lengo la kuwa na walimu hao ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike wanapatiwa elimu ya afya na usafi itakayowawezesha kutambua mabadiliko yanayotokana kupevuka kwa miili yao.

Aidha,wanafunzi hao wanahitaji mlezi wa kuweza kuwasaidia wanapokuwa na changamoto mbalimbali kuhusiana na masuala ya kike.

Naibu Waziri huyo alisema Serikali kupitia Mpango wa Lipa Kutokana na Matokeo (EP4R) imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kusawazisha ikama ya walimu wakiwemo walimu wa kike katika Halmashauri ili kukabiliana na tatizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles