27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima watakiwa kuangali kilimo biashara

ASHA BANI– DAR ES SALAAM

BARAZA la Kilimo nchini (ACT), limewataka wakulima kulima kilimo cha biashara na uhifadhi wa mazingira ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yalielezwa juzi jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wa baraza hilo, Dk. Jacqueline Mkindi wakati akielezea majukumu yaliyofanikishwa pamoja kongamano na maonyesho yanayotarajia kufanyika Februari 27 na 28 katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini hapa.

Alisema hali ya sasa ni mbaya kwa wakulima kama ambavyo wengi wameshuhudia kutokana na kuwa na msimu wa mvua zisizo tabirika.

Baraza hilo pia lilizungumzia suala la kudhibiti Nzige waharibifu wa masao ambao tayari wamepiga hodi nchi jirani ya Kenya.

“Tumezungumza pia na Taasisi ya Utafiti ya TARI na kuona ni jinsi gani ambapo tatizo hilo likiingia nchini tunaweza kulidhibiti hivyo tahadhari ni muhimu kwetu wadau wa kilimo,” alisema Dk.Mkindi.

Aliongeza kuwa Baraza la Kilimo lililoanzishwa mwaka 1999 lilizinduliwa mwaka 2000 na Rais Benjamin Mkapa na kufanya mengi ambayo ni mafanikio ya taasisi hiyo.

Alisema baraza ndilo lililofanya mchakato wa kupatikana kwa Benki ya Wakulima, suala ambalo alisema wamelipigania na kuwasaidia wakulima kupata mitaji kwa urahisi.

“Baraza limeshawishi serikali kufanyia marekebisho sera ya kilimo ya 2013 ili kuwepo na kipengele cha kulinda ardhi ya kilimo kisheria na pia usajili wa wakulima,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles