31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wa ndizi waiangukia Wizara ya Kilimo

Safina Sarwatt -Rombo

WAKULIMA wa ndizi Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, wameomba Wizara ya Kilimo kuwapatia   pembejeo ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa zao hilo.

Wakulima hao, walisema kuwa kilimo cha ndizi kina soko kubwa kuliko kahawa na kwamba changamoto kubwa ni upatikanaji wa mbegu bora za migomba.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani hapo jana, walisema wanashindwa kuzalisha ndizi zenye ubora, licha ya kuwapo soko la uhakia.

Ansila Lyimo, alisema uzalishaji wa zao hilo ni mdogo kutokana na wengi wao kuzalisha ndizi kwa chakula na si biashara, licha ya zao hilo kwa sasa kuonekana kufanya vizuri  baada ya kilimo cha kahawa kukosa soko.

Mtaalamu wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari), Juma Kitundu, alisema Serikali imeanza mpango wa kuwezesha wakulima wa ndizi kuboresha kilimo  ili kuongeza uzalishaji wa ndizi bora zitakazokidhi soko la ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na wakulima hao, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo, alisema sasa zao hilo ndilo la kibiashara baada ya mazao mengine kukosa masoko ya uhakika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles