WAKULIMA WA CHAI LUSHOTO WALIA NA UKATA

0
2

Wakulima wa chai wilayani Lushoto, wamedai wanashindwa kumudu gharama za maisha ikiwamo kusomesha watoto baada ya Kiwanda cha Chai cha Mponde, kilichopo Lushoto mkoani Tanga kufa.

Kutokana na hali hiyo, chai wanayolima sasa inakosa soko kwani kiwanda hicho kilikuwa ni miongoni mwa wanunuzi wakubwa wa zao hilo.

Hayo yamebaiinishwa leo jijini Tanga na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli, Amir Abdalah Shuza, wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tanga (RCC).

“Awali wakulima hao walitegeme kiwanda hicho kwa kuuza chai yao ambapo kwa sasa hali ni tofauti wananchi wengi wamepoteza matumaini ambapo wakulima hao wamekosa soko madhubuti hali inayowafanya kulalamika ugumu wa maisha.

“Aidha, kukosekana kwa kiwanda hicho kumesababisha chai kukosa soko jambo ambalo wakulima wanaomba serikali iwatafutie mwekezaji mwingine kutokana na chai wanayolima kuozea mashambani,” amesema Shuza.

Akijibu hoja hiyo, Mkuu wa Mkoa Tanga, Martine Shigella ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho amesema serikali imeiona changamoto hiyo na utaratibu wa kumaliza tatizo hilo unafanyika.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here