24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima tumbaku wapata viongozi wapya wa bodi

Na ALLAN VICENT – TABORA

CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) kimepata viongozi wake wapya wa bodi, huku Mrisho Simba akichaguliwa kuwa mwenyekiti.

Uchaguzi wa viongozi wa bodi hiyo ulifanyika juzi mjini hapa chini ya usimamizi wa Mrajisi Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika Tanzania, Sadick Chibila.

Akitangaza ushindi wa Simba ambaye ni mjumbe kutoka Wilaya ya Uyui, Chibila alisema kiongozi huyo mpya alipigiwa kura na wajumbe wote 183.

Pia mjumbe kutoka Wilaya ya Sikonge, Nuru Maziku alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo baada ya kupigiwa kura 182 na wajumbe wa mkutano huo.

Aliwataja wajumbe watano waliochaguliwa kuingia katika bodi hiyo kuwa ni Erick Kissa kutoka Kitunda (Sikonge), Ali Shaban kutoka Manispaa ya Tabora, Salumu Mrisho kutoka Wilaya ya Nzega, Mariamu Juma na Abdallah Issa kutoka Uyui.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Simba alisema kuwa atahakikisha kila mkulima ananufaika na jasho lake, aidha alionya viongozi wa vyama vya msingi wasio waadilifu kuacha mara moja tabia hiyo vinginevyo watachukuliwa hatua kali.

Aliahidi kuimarisha ushirika, kukomesha urasimu, kusimamia haki za wakulima na kukomesha vitendo vya ubadhirifu vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi wenye tamaa na uchu wa mali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles