30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima kuonana na Waziri Mkuu Dodoma

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA

WAKULIMA zaidi ya 70 wa mpakani mwa Kongwa mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara, wamefanya maandamano ya amani kwa lengo la kuonana na Waziri Mku, Kassim Majaliwa,   wamueleze kilio chao cha kuporwa maeneo yao ya kilimo.

Wakulima hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nalau kijiji cha Kiteto Kata ya Lenjulu, Daimon Chimulu, walisema   wamelazimika kufanya maandamano kutoka wilayani Kongwa hadi Dodoma kuonana na Waziri mkuu   kumueleza kero zao za kuporwa mashamba yao ya Lumilumi na kutaka maeneo hayo yatumiwe na wafugaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti huyo alisema   pamoja na kufanya maandamano kwa ajili ya kuonana na Waziri Mkuu aweze kutatua mgogoro walionao, juhudi zao za kuonana naye zimegonga mwamba kutokana na kutokuwapo ofisini kwake.

Mwenyekiti huyo alisema kilio chao   ni kutaka kupewa mashamba yao  waweze kuendelea na shughuli zao za kilimo kwa vile  kwa sasa hawajui hatma ya maisha yao ingawa wapo katika maeneo hayo kwa muda mrefu.

“Sisi wakulima wa eneo la Lumilumi tunahitaji kujua hatma yetu kwa sababu  tumezuiliwa kufanya shughuli zetu za uzalishaji kwa maana ya kilimo na tumeambiwa tusifanye shughuli yoyote ya kilimo wala wafugaji wasiingize mifugo katika maeneo hayo.

“Jambo la kushangaza kwa sasa tumekuwa tukiona mifugo ikiingia katika maeneo yetu na kula mazao yetu jambo ambalo lisasababisha kuwapo   viashiria vya machafuko au kutoweka   amani kutokana na mgogoro huo.

“Imefikia hatua ya wafugaji   kuanza kuwashambulia wakulima kwa fimbo huku hakuna hatua yoyote ya  sheria ikichukuliwa,” alisema Mwenyekiti huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles