24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wakala wa wachezaji kusajiliwa TFF

Na Johns Njozi



Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) limetoa fomu maalumu kwa wale wanaohitaji kuwa mawakala wa wachezaji wa mpira wa miguu.

Msemaji wa shirikisho hilo Clifford Ndimbo, amesema fomu hizo zinapatikana kwenye ofisi za (TFF) na tovuti ya shirikisho hilo na mtu anayetaka kuwa wakala wa mchezaji anapaswa kujaza fomu hizo ili aweze kupata kibali cha kufanya shughuli hizo.

“Kwa wale mawakala wa wachezaji tunaofahamu kwamba taratibu zimebadilika kwa hiyo utaratibu mpya ndio tunaanza kuutumi na tayari fomu zimeanza kutolewa.

Lakini moja kati ya vitu vinavyo kamilisha fomu hiyo kukamilika ni pamoja na ripoti ya Interpol ambayo itasaidia kujua masuala mbali mbali ya atakayejaza fomu,” alisema Ndimbo.

Ndimbo ameongeza kwamba gharama za kupata kibali ni dola za kimarekani 2000 zaidi ya shilingi milioni nne za kitanzania kwa miaka miwili na baada ya hapo itakuwa inalipiwa dola za marekani 500 kila baada ya mwaka ambazo ni zaidi ya shilingi milioni moja za kitanzania kama ada ya kubadilisha kibali hicho kitakapoisha muda wake.

Fomu hizo zinazopatikana kwenye tovuti ya (TFF), zinajazwa mtandaoni na mwisho wa kujaza na kuzirejesha fomu hizo ni Decemba, 30 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles