25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAJUMBE WAIDHINISHA USHINDI WA TRUMP

WASHINGTON, MAREKANI


donald-trumpWajumbe wa jopo la wateule wanaoamua ushindi wa rais wa Marekani, wamemwidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 8, mwaka huu.

Hatua hiyo imezima juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia Trump kuingia ikulu ya White House Januari 20.

Baada ya ushindi huo, Trump ameahidi ‘kufanya kazi kuunganisha nchi yake na kuwa rais wa Wamarekani wote’.

Wajumbe walikuwa wametumiwa ujumbe kupitia barua pepe na pia kupigiwa simu wakihimizwa kutomuunga mkono bilionea huyo kabla kukutana kupiga kura.

Shughuli yao ya kupiga kura kwa kawaida huwa kama ya kutimiza wajibu tu, huwa wanamuidhinisha mshindi. Lakini mwaka huu uchaguzi umegubikwa na tuhuma za kuingiliwa na wadukuzi kutoka Urusi, huku mshindani wa Trump, Hillary Clinton, akiongoza kwa kura za kawaida kwa pengo la kura milioni 2.5.

Jimbo la Texas hatimaye lilimuwezesha kufikisha idadi ya kura 270 za wajumbe alizohitaji, licha ya wajumbe wake wawili kugeuka na kupiga kura kumpinga.

Matokeo ya kura hiyo yatatangazwa rasmi Januari 6 katika kikao maalumu cha pamoja cha Bunge la Congress.

“Nawashukuru Wamarekani kwa kunipigia kura kwa wingi kuwa rais wa Marekani,” alisema Trump kupitia taarifa baada ya matokeo kutangazwa.

“Kwa hatua hii ya kihistoria, tunaweza sasa kutazama mbele na kutarajia maisha ya kufana siku za usoni. Nitafanya kazi kwa bidii kuunganisha nchi yetu na kuwa rais wa Wamarekani wote,” alisema.

Iwapo kungetokea iwe kwamba hakuna mgombea aliyefikisha kura 270 za wajumbe, Bunge la Wawakilishi ndilo lingekuwa na jukumu la kuamua nani angekuwa rais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles