29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wajipanga kuulinda mmea unaoongeza nguvu za kiume

Francis Godwin, Mbeya 

Wadau wa mazingira wanaozunguka   Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wilayani Makete   mkoani Njombe wameanza mkakati wa  kuulinda mmea wa chikanda usitoweke.

Mmea huo unadaiwa kuongeza nguvu za kiume na unasaidia wagonjwa walioathirika na Virusi Vya Ukimwi (VVU),umedaiwa kuwa hatarini kutoweka kutokana na kuingiliwa na majangili.

Diwani wa Kata ya Kitulo, Abel Mahenge,  amesema baadhi ya watu nchini na nchi jirani kama Zambia na Malawi, wamekuwa  wakijihusisha na vitendo vya ujangili ndani ya  hifadhi hiyo wakiwinda mmea huo ambapo  huchimba  na  kuondoka na kiazi chake  wakiamini ni dawa.

Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Itundu Wilaya ya Makete, Eva Ngombe amesema kupitia kikao hicho cha pamoja cha ujirani mwema wao watakuwa chachu ya ufikishaji elimu kwa jamii  juu ya uhifadhi na ulinzi wa hifadhi ya Kitulo na hata  kuchukua  hatua  dhidi ya vitendo vya ujangili ndani ya hifadhi   hiyo.

“Ili kuendelea kulinda hifadhi na mmea wa chikanda kuendelea kubaki salama bila  kuvamiwa na majangili, tumejiwekea  utaratibu wa kulinda Hifadhi ya Kitulo kwa  ulinzi shirikishi dhidi ya ujangili na uvamizi wa aina yoyote ile,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles