27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WAJERUMANI WASHAURIWA KUTEMBEA KAMA PENGWINI

Akifundishwa kutembea kama Pengwini katika barafu
Akifundishwa kutembea kama Pengwini katika barafu

MADAKTARI nchini Ujerumani wamewashauri raia nchini humo kutembea kama ndege aina ya pengwini (penguin) kwa lengo la kuepuka kuteleza na kuanguka katika kipindi hiki cha baridi kali.

Ni kwa sababu kipindi hiki kinaandamana na kuanguka kwa theluji ambazo baadae huganda na kuwa barafu katika maeneo mengi ya barabara.

Kitengo cha utabiri wa hali ya hewa nchini humo kimesema hali hiyo itaendelea kwa siku kadhaa na kwamba ni aina hiyo ya utembeaji inayomsaidia kiumbe huyo anayeishi katika maeneo ya baridi kali inayoweza kuwanusuru watu na hatari ya kuvunjika viungo vyao.

Ushauri huo uliosambazwa kupitia tovuti ya chama cha watoa tiba ya mifupa nchini Ujerumani na ushauri na nasaha unasema kutembea kwa kunyata kunakofanywa na aina ndege huyo, kunaweza kusaidia kukabiliana na kuteleza katika barabara zenye barafu.

Lakini kama binadamu atatembea kwa namna yake ya kawaida ni rahisi kuteleza na kuanguka.

Manispaa ya Berlin ilikosolewa vikali mwaka 2014 kwa kushindwa kumwagia chumvi maalumu zenye kusaidia kuyeyusha barafu katika njia nyingi, na hivyo kusababisha idadi kubwa ya watu kuteleza na kuumia.

Timu ya uokozi katika jiji hilo ilipokea simu za dharura 750 na vyumba vyake vya matibabu vilikabiliwa na idadi kubwa ya watu wenye matatizo ya mifupa.

Na kwamba utabiri wa hali ya hewa wa sasa unaonesha kiwango cha joto kitashuka hadi kufikia nyuzi joto -10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles