24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wajasiriamali wazililia taasisi za fedha

tanzanian-shillings

Na MASANJA MABULA, PEMBA

TAASISI zinazotoa mikopo nchini, zimetakiwa kuwasaidia wajasiriamali wadogo walioko vijijini kwa kuwapa mikopo yenye masharti nafuu isiyokuwa na riba.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mjasiriamali aliyejitambulisha kwa jina la Dadi Hamad Dadi, mkazi wa Madenjani, Wilaya ya Wete, Pemba, alisema kama wakipata mikopo kwa masharti nafuu, watakuza mitaji yao kwa haraka tofauti na ilivyo sasa.

“Mimi biashara yangu ni kuuza maembe ya kukausha, lakini pamoja na ubunifu wangu huo, taasisi zinazotoa mikopo zimeshindwa kutambua mchango wangu katika kukuza pato la taifa na kuzalisha ajira kwa vijana.

“Kwa hiyo, naiomba Serikali iangalie namna ya kuzishawishi taasisi za fedha ziweze kutoa mikopo kwa riba nafuu ili tuweze kukuza mitaji yetu kwa haraka,” alisema Dadi.

Kwa mujibu wa Dadi, yeye binafsi anahitaji mikopo ya aina hiyo kwa kuwa licha ya bidhaa anazozalisha kuwa na soko la uhakika nchini Kenya, ameshindwa kulitosheleza soko hilo kutokana na kutumia vifaa duni na ambavyo vinashusha ubora wa bidhaa hiyo.

Naye Diwani wa Kata ya Kiungoni, Mussa Hossein Ayoub, aliahidi kulishawishi Baraza la Madiwani ili liangalie njia za kuifanya Serikali iingilie kati suala la mikopo yenye masharti nafuu kwa wajasiriamali.

“Sisi kama wasimamizi wa Serikali za Mitaa, tunapaswa kuunga mkono juhudi za wajasiriamali wadogo walioonyesha nia ya kupambana na umasikini,” alisema Ayoub.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mji wa Wete, Assa Juma Ali, aliunga mkono hoja hizo na kuwataka wajasiriamali wasikate tamaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles