28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wajasiriamali watakiwa kurasimisha biashara zao

 Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema ni  lazima kwa wafanyabishara  wakati  na wadogo nchini kurasimisha biashara zao  ili iwe rahisi kutambulika kitaifa na kimataifa.

Akizungumza na Mtanzania Digtal leo Juni 10, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa BRELA,  Bakari Mketo amesema Tanzania ina wajasiriamali wengi ambao bado hawajarasimisha biasahara zao.

Ameisema kuna faida nyingi sana kwa wajasiriamali kurasimisha biashara  ambazo  ni kuwasaidia kuwapa  kitambulisho na leseni, wakati nchi huu ambao inaelekea katika uchumi wa viwanda  lazima biashara zote nchini ziwe zimerasimishwa.

Amesema kuwa kurasimisha  biashara ni kuipa kitambulisho ambacho ni muhimu sana kwasababu ili mfanyabiashara aingie  katika ushindani wa tenda za kazi  lazima awe amesajiliwa BRELA na kama  biashara  au kampuni haijasajiliwa haitakuwa na sifa.

Naye Msajili Msaidizi wa Kitengo cha Ubunifu wa BRELA, Suzan Senso amesema changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa wafanyabishara kutokana na kwamba kwa upande wa  Vikoba na Saccos  wakisajiliwa kwa maendeleo ya jamii basi wanajua wamemaliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles