31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waitara: Walimu wasidai nyongeza ya mshahara kama haijatolewa

Arodia Peter, Dodoma

Serikali imesema walimu hawapaswi kudai nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa miaka ambayo nyongeza hiyo haikutolewa.

Hayo yamesemwa bungeni leo, Ijumaa Mei 10, na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Mussa Bakar (Chadema).

Katika swali lake Zainabu aliuliza; “Walimu nchini wameingia mkataba na mwajiru wao ambao pamoja na mambo mengine unaonyesha uwepo wa nyongeza ta mshahara kila ifikapo Julai, lakini tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani hawajapewa stahiki hizo, je ni lini walimu watalipwa malimbikizo hayo?”

Katika majibu yake, Waitara alisema Serikali imekuwa ikitekeleza miongozo mbalimbali kuhusu maslahi ya walimu zikiwamo nyongeza za mwaka za mishahara kulingana na utendaji wa mhusika na tathmini ya kila mwaka.

“Kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni ya kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009 toleo la tatu, nyongeza ya mwaka ya mshahara haipaswi kuombwa au kudaiwa na walimu, bali serikali ndiyo yenye uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza hiyo kutokana na sera za kibajeti kwa mwaka husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles