Imechapishwa: Fri, Nov 10th, 2017

WAHU AKIMBILIA KUIMBA INJILI

NAIROBI, KENYA


STAA wa filamu na muziki nchini Kenya, Rosemary Kagwi ‘Wahu’, ameamua kukimbilia kwenye muziki wa Injili baada ya mapema wiki hii kuachia video ya wimbo wake mpya wa kumsifu Mungu uitwao Sifa.

Msanii huyo amesema amefanya maamuzi ya kuimba aina hiyo ya muziki kutokana na kuamini kuwa maisha kuna wakati yanapanda na wakati mwingine yanashuka, hivyo ni vizuri kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

“Maisha yana mambo mengi, si tu kwa wasanii ni kila mtu duniani, hivyo ni vizuri kumshukuru Mungu kwa kila jambo kwa kuwa yeye ndiye kila kitu.

“Nimepitia aina mbalimbali ya maisha, kuna wakati mambo yangu yalikuwa magumu, lakini nilimuomba Mungu na akanisaidia, kutokana na hali hiyo nikaona ni bora kumsifu yeye kwa kuwa ndiye anayepanga,” alisema Wahu.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

WAHU AKIMBILIA KUIMBA INJILI