27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa wa corona wanne wafariki, 15 wakipata maambukizi Kenya

 NAIROBI, KENYA

KENYA imeripoti jumla ya visa 411 vya maambukizi ya virusi vya corona jana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na Waziri wa Afya wan chi hiyo Mutahi Kagwe, watu 15 zaidi wamepatikana na virusi vya corona kufuatia uchunguzi wa vipimo vya sampuli 1,434 vilivyofanywa saa 24 zilizopita.

Kenya ambayo ilithibitisha kupata maambukizi ya kwanza ya corona mwezi Machi, imekwishapima sampuli 21,702 kutoka maeneo mbali mbali ya nchi hadi kufikia Mei 1.

Waziri huyo wa afya amesema idadi ya watu waliopona virusi vya corona imepanda na kufikia watu 150 huku sita zaidi wakiruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona.

Mutahi amesema idadi ya vifo vilivyosababishwa na Covid-19 imefikia watu 21 baada ya wagonjwa 4 zaidi kufariki dunia.

Kufuatia kutangazwa kwa upimaji wa jumla katika maeneo ya nchi, wizara imefanya shughuli hiyo katika eneo lenye msongamano wa watu wengi la Kawangware jijini Nairobi siku ya Ijumaa.

Lengo la shughuli hiyo ni kuwabaini na kuwatenga watu walioambukizwa na kutafuta watu waliokutana nao ili kuzuwia kusambaa zaidi kwa virusi vya corona.

Wakati huohuo, Kenya imepokea karibia vifaa 40,000 vya kupimia ikiwa ni katika kuimarisha hatua za uwezo wa kupima watu kunakoendana na lengo la kupima, kutengwa walioathirika na kutibu.

Wizara ya afya imetangaza Jumatano kwamba nchi hiyo imepokea vifaa vya kupimia mfano wa vijiti 18,900, vifaa vya kuwekea vipimo 18,912, sare na vifaa vya kujikinga kwa wahudumu wa afya 3,790, vipimajoto vya kushikililiwa, glavu na mashine za kupuma kutoka kwa mfanyabiashara wa kundi la Alibaba, Jack Ma.

Waziri amesema Kenya pia ilikuwa imepokea shehena ya glavu, vifaa vya kujikinga kwenye uso na barakoa zinazovaliwa wakati wa upasuaji kutoka China, Ufaransa na Ujerumani kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO).

Baadhi ya hatua zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta kufuatia janga la corona huko nyuma ni pamoja na:

1.Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

2. Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19

3. Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takribani miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.

 4. Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitasaidiwa kutokana na fedha zilizotengwa na serikali kusaidia familia zisizojiweza

5.Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.

6. Ili kuhakikisha msaada unagawanywa kwa njia salama, mfuko wa hali ya dharura wa kukabiliana na Covid-19, Kenya na mashirika mengine ya usalama yatashirikiana kuratibu miradi kama ule wa Adopt a Needy Family, ambapo raia wa Kenya wanasaidiana kipindi hiki cha janga kuhakikisha hatua zinachukuliwa bila kufuata urasimu

7.Afisa yeyote wa polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles