Imechapishwa: Fri, Aug 11th, 2017

WAGONJWA WA AKILI WAIBIANA NGUO ZA NDANI

Na OSCAR ASSENGA-KOROGWE

MUUGUZI Msaidizi wa Hospitali ya Afya ya Akili na Utengamao ya

Lutindi iliyoko wilayani Korogwe, Mkoa wa Tanga, Amina Ramadhani, amesema wagonjwa wa akili wanaolazwa hospitalini hapo wamekuwa wakiibiana vitu mbalimbali zikiwamo nguo za ndani.

Kutokana na hali hiyo, amesema uongozi wa hospitali hiyo umekuwa ukiwatenga kwa baadhi yao ambao pia huwa wanapigana na kuumizana.

Kwa mujibu wa Amina, wagonjwa hao hupigana baada ya kuibiana vitu mbalimbali zikiwamo nguo za ndani, sabuni, mafuta na dawa za meno.

Amina aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hospitali hiyo ili kuangalia huduma zinavyotolewa.

“Wagonjwa wamekuwa mara kadhaa wakipigana baada ya kuibiana vitu mbalimbali na inapotokea hivyo, tunalazimika kuwatenga ili wengine waweze kuishi kwa amani.

“Kwa hiyo inapotokea hali kama hiyo, wananchi wakiwamo ndugu wa wagonjwa wajue tunafanya hivyo kwa nia njema ili kuokoa maisha ya wagonjwa wetu,” alisema Amina.

Awali, akizungumzia suala hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Katyetye Marwa,

alisema idadi ya wagonjwa wa akili nchini imeongezeka na kufikia asilimia 30 kutokana na ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya.

“Takwimu hizo zinaonyesha namba ya watumiaji wa dawa za kulevya kwa bangi na heroin zimekuwa juu sana kwa kuwa zinauzwa kwa bei rahisi kuliko chakula.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

WAGONJWA WA AKILI WAIBIANA NGUO ZA NDANI