27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wagombea wategana uchaguzi Yanga

Aloyce KombaNA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

ZOEZI la uchukuaji fomu za kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga, limeonekana kusuasua baada ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kutojitokeza kuchukua fomu hizo.

Mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Yanga ulianza rasmi jana kwa wagombea kutakiwa kwenda kuchukua fomu ya kuomba kuwania nafasi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Juni 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Aloyce Komba alisema baadhi ya wanachama wamejitokeza kwa wingi katika ofisi za shirikisho hilo lakini hawakuchukua fomu hizo.

“Wanachama wengi tu wamekuja leo (jana) na baadhi ya viongozi pia walituma wapambe wao, lakini hakuna hata mmoja aliyechukua fomu, wengi walisema kuwa wamekuja kuhakikisha kama kweli zimeanza kutolewa,” alibainisha Komba.

Aidha, Mwenyekiti huyo aliwataka wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu hizo na kutoa wito kwa wale wote ambao hawajalipia kadi zao kufanya hivyo ili waweze kupiga kura kihalali.

“Wanachama wajiandae, wasiolipia kadi zao wakazilipie ili waweze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka, wawe hai, hii itasaidia uchaguzi kuwa huru na wa haki,” alisema.

Gharama ya fomu itakuwa ni Sh 200,000 na kwa nafasi nyingine za wajumbe Sh 100,000 huku mwisho wa kurejesha fomu hizo ni Mei 31 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles