23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waganga wakuu watakiwa kuboresha magodoro

Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

SERIKALI imewataka waganga wakuu wa mikoa na wa halmashauri kuhakikisha ndani ya wiki mbili kuanzia sasa, wawenunua vitambaa vigumu vya mpira ambavyo hutumika kufunika magodoro yanayotumiwa na wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili yasiharibike kirahisi.

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya, Dk. Dorothy Gwajima alipofanya ziara kutembelea  hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni  jijini Dar es Salaam.

Alitoa  siku 14 kuanzia sasa kwa waganga hao kuhakikisha  magodoro yaliyopo kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati kwenye mikoa yao yanashonwa na kuwekea mifuko maalumu ya mpira ili kuyafanya yarudi katika ubora wake.

Alisema kumekuwa na mtindo kwa baadhi ya watendaji wa halmashauri  kusingizia uchakavu wa magodoro na vitanda kwa vile tu Bohari Kuu ya Dawa  (MSD)ili ipeleke magodoro yenye vitambaa laini vya mpira na ni siku nyingi tangu  magodoro hayo yaletwe.

“Watendaji wengine wamekuwa wakidai  MSD wametuuzia magodoro haya siku nyingi na kitambaa chake laini hivyo yameanza kuchoka,”amesema na kuongeza.

“Wakati inawezekana kununua kitambaa cha mpira, kwenye maduka yaliyopo yanayouza vitambaa vya mpira, mafundi wapo na kwa kuwatumia mafundi wenyeji wakashona magodoro haya yakarudi kuwa  mapya,” alisema.

Alisema hakuna sababu kwa watendaji hao kutumia visingizio vyao, kwani bei ya kununulia mita kadhaa za vitambaa vigumu vya mpira  na za mashono ni ndogo na ni gharama zilizo ndani ya uwezo wa vituo vyetu vya kutolea huduma za afya.

Wakati huo huo, Dk. Gwajima alisifia hatua ya uongozi wa hospitali ya Vijibweni i kuamua kukopa mashine ya Xray kutoka MSD ili  kuwahudumia wananchi  wengi.

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa misongamano ya  wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, Dk.Gwajima amesema pamoja na ukweli kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na upungufu wa watumishi, yapo baadhi ya maeneo ambayo upungufu huo unachangiwa na uzembe wa baadhi ya watoa huduma katika kuwajibika.

 “Baadhi ya wataalam huwa wanachelewa kufika kazini na wakifika wanaishia kuona idadi ndogo ya wateja chini ya kiwango cha walau wateja 30 hadi 40 kwa siku kilichopo kwenye miongozo,” alisema.

 “Kupitia utaratibu wa kupima uwingi wa kazi kwa wakati wa sasa (workload) inawezekana kuchochea uwajibikaji wa mtumishi mmoja mmoja na kuleta uwiano sawa wa kazi miongoni mwa watumishi wa vituo mbalimbali na siyo baadhi wanasema kuna upungufu wa watumishi akiulizwa amehudumia wateja wangapi unakuta hata kumi hawafiki,” alisema.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Yudas Ndungile alisema   wamepokea maagizo ya Dk. Gwajima yatatekelezeka kwa vile yapo ndani ya uwezo wa mkoa wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles