31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wafungwa walioachiwa wasirudie makosa

RAIS Dk. John Magufuli juzi ametangaza msamaha wa wafungwa 5,533 kwa mamlaka aliyonayo kikatiba.

Rais Dk. Magufuli alitangaza msamaha huo wakati wa sherehe za 58 ya Uhuru wa Tanganyika na 57 ya Muungano kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Kwa maelezo yake, alisema alipotembelea gereza la Butimba mkoani Mwanza mapema mwaka huu, alijionea msongamano mkubwa wa wafungwa na mahabusu jambo ambalo lilimfanya aviagize vyombo vya dola kufanya kazi ya uhakiki.

Alisema hadi sasa kuna wafungwa 17,547, mahabusu 18,256 jumla kuu ikiwa ni 35,803 idadi ambayo ni kubwa.

Lakini cha kusikitisha, rais anasema wapo wafungwa waliofungwa kwa makosa madogo madogo  kama ya kuiba kuku, kujibizana vibaya na wepenzi wao, kushindwa kulipa faini na wengine kuonewa.

Hakika anasema alihuzunishwa na hali hiyo, hakuna binadamu mkalimifu kwa sababu wote wanamkosea Mungu na wengi walitubu.

Tunakubaliana na kauli hii kuwa wapo wafungwa wengi ambao walibambikiziwa kesi na  vyombo vya dola kwa utashi wao na jambo hili limeumiza watu wengi mno.

Tunasema hivyo kwa sababu, mmoja wa wafungwa aliyeachiwa  katika gereza la Isanga mkoani Dodoma,  Adullah Ramadhan (55) mkazi wa Kata ya Ibaga wilayani Mkalama  Mkoa wa Singida anasema alifungwa miaka 30 kwa kuonewa.

Anasema yeye alikuwa an kosa la kuingiza mifugo kwenye shamba za mtu, lakini cha kusangaza alibambikiziwa kesi ya kubaka, kitu ambacho hakuwahi kukifanya.

Mfungwa huyo alifungwa akiwa na umri wa miaka 35 mwaka 2000, ametoka jana akiwa na umri wa miaka 55, huku akilia kwa uchungu baada ya kuwambia mkewe wake wametangulia mbele ya haki.

Si nia yetu kueleza mambo mengi, lakini wakati tunawashauri wafungwa walioachiwa jana, kuwa raia wema  waendako, tunavihisi pia vyombo vya dola vibadilike na kuachana na tabia ya kubambikizia watu kesi.

Tunaamini sasa wafungwa wote watakuwa mabalozi wema kufanya kazi kwa bidii kutokana na mafunzo ambayo wameyapata wakati akiwa gerezani. Ufundi huo uwe mwanzo wa wao kujiajiri na kujipatia kipato halali mbele ya jamii

Ni mategemeo yetu watafanya kazi japo wanaanza kwa mazingira magumu ya kupata mitaji, kikubwa ni kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.

Kila mmoja atashiriki ujenzi wa taifa kwa kufanya na kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda kama ambavyo Rais Dk. Magufuli amekuwa akinena kila siku

Tunategema kila mfungwa atatenda kila jambo kwa kuzingatia kanuni,taratibu na Katiba ya nchi ili wasirudiwe makosa.

Ni ukweli usiopingika wafungwa wote hawana bodi kwenda na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji kama walivyofundishwa wakati wakiwa gerezani kipindi chote walichokuwa wanatumikia adhabu zao.

Wafungwa wengi wamekuwa wakipata mafunzo mbalimbali ya ujenzi, kilimo na kazi za mkono kama ufumaji wa vitambaa na vikapu, hivyo waendee wakasimamie ujuzi wao.

Pamoja na hayo, tunasihi vyombo vya dola hasa jeshi la polisi kubadilika katika suala na kuacha mwenendo wa kubambikizia watu makosa yasiyokuwa na tija. Jambo hili limeonekana wazi kuumiza Rais Dk. Magufuli hadi kufikia uamuzi wa kutoa msamaha mkubwa huu ambao haujawahi kutolewa miaka yote.

Tunasisitiza hili kwa sababu polisi ndiyo waandaa mashtaka na kuyapeleka mahakamani, umefika wakati wabadilike na kuachana na tabia hii ambayo inaumiza watu kila kukicha. Tunamalizia kwa kusema wafungwa wote mlioachiwa msirudie makosa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles