24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAFANYAKAZI MIGODINI KAHAMA WAANDAMANA


Na PASCHAL MALULU    |

WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Uchimbaji dhahabu ya Acacia wa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi wilayani Kahama wameandamana hadi ofisi za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakitaka kulipwa sitahiki zao baada ya kuondolewa kazini.

Hali hiyo ilitokea jana baada ya wafanyakazi hao kuandamana wakipita mitaa kadhaa ya Mji wa Kahama hadi ofisi za NSSF wakidai kulipwa mafao yao kutokana na madai yao kuwa ya muda mrefu.

Mmoja wa wafanyakazi waliondamana, Ismail Hamza alisema kabla ya kuondolewa kazini walielezwa na meneja wa mgodi ambaye hakumtaja jina kuwa malipo yao ya mafao yako tayari.

Hamza alisema meneja huyo aliwaeleza kuwa waliwasiliana na NSSF ambao waliwaahidi baada ya wiki tatu wangelipwa lakini hadi sasa miezi mitano imepita hawajalipwa.

Alisema wamekuwa wakifika katika ofisi za NSSF mara kadhaa lakini walishangazwa na kauli ya watumishi wa shirika hilo aliyedai hawataruhusiwa kuchukua malipo yao kutokana na hisia  kwamba wangezitumia vibaya fedha zao.

Hamza alisema walilalamikia kauli hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu ambaye aliwasaidia kufungua akaunti zitakazotumika kulipia malipo yao.

Naye Julius Msofe alisema kabla ya kuondolewa kazini wafanyakazi wote waliitwa NSSF na kusajiliwa ili isitokee ucheleweshaji wa malipo yao lakini hadi sasa mwezi wa tano hakuna malipo yoyote .

Akizungumzia hali hiyo, Meneja  wa NSSF mkoa Maalumu wa Kahama, Wiston Mdingile alisema wameshindwa kuwalipa kwa pamoja wafanyakazi hao kutokana na migodi hiyo kuwapunguza watumishi wengi kwa wakati mmoja.

Mdingile alisema hali hiyo imesababisha kufunguliwa kwa madai mengi kwa pamoja ambayo hawamudu  kuyalipa kwa wakati.

Alisema wafanyakazi wanaostahili kulipwa ambao wamefungua akaunti za madai ya mafao yao ni zaidi ya 2000 lakini waliokwisha kulipwa ni karibu nusu yake.

Meneja huyo alisema wamekuwa wakiwalipa kwa awamu kulingana na waliotamgulia huku akiwaomba wafanyakazi wengine kuwa wastahimilivu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles