24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAFANYABIASHARA WA MBAO WAMVAA MBUNGE, TANESCO

Na PASCHAL MALULU-SHINYANGA

WAMILIKI wa viwanda vya mbao wa  Bukondamoyo waliopo Kata ya Mhungula Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, wamemtaka Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Jumanne Kishimba, kusimamia Shirika la Tanesco wilayani humo ili waweze kuhamisha mita zao katika eneo la zamani na kuzipeleka walikohamishiwa.

Wafanyabiashara hao walihamishwa Juni mwaka huu kwenda eneo la Bukondamoyo ambako ndiko eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo vya mbao ambapo wanalalamikia kitendo cha kutopelekewa mita ili shughuli zao ziweze kuendelea kama ilivyokuwa awali.

Mmoja wa wamiliki wa viwanda hivyo, Hussein Salum, alimtupia lawama mbunge wa jimbo hilo akidai kuwa analitambua tatizo linalowakabili lakini  ameamua kuwatelekeza huku akimwachia majukumu yote katibu wake, Abdul Mpei, ambaye hana uwezo wa kuwasaidia.

Naye Katibu wa tume iliyoundwa na wamiliki wa viwanda hivyo, Mohamed  Kihiga, alisema licha ya Serikali kujitahidi kufikisha nguzo za umeme katika eneo la viwanda vya mbao ambapo inadaiwa mita za umeme 28  hazikuruhusiwa kuhama hadi maombi yatumwe upya.

Alisema wao hawaoni uhalali wa kuomba mita mpya kwa kuwa  wakati wanaondolewa katika eneo hilo hawakuelezwa suala la mita zao kutotumika katika eneo jingine.

Alisema wanasikitishwa na kitendo cha mita zao kuzuiliwa wakati zilichukuliwa na salio kati ya Sh 150,000 hadi 300,000, hivyo ni vema wakarejeshewa.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Tanesco Tawi la Kahama, King Fokanya, alipohojiwa na madiwani hao juu ya kuwanyima mita zao wafanyabiashara, alisema sheria na taratibu za shirika haziruhusu mteja kuhama na mita yake kuhamishia sehemu nyingine huku akieleza kuwa hadi hapo atakapopata mwongozo wa ngazi ya mkoa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles