27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara Mwanza wagoma

Jiji la Mwanza
Jiji la Mwanza

SITTA TUMMA NA PETER FABIAN, MWANZA

WAFANYABIASHARA jijini hapa wamegoma. Mgomo huo ulianza jana asubuhi baada ya wafanyabiashara hao kusitisha huduma zote kwa kile walichoeleza kuwa ni kutoridhishwa na gharama za ushuru wanazotozwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Mgomo huo unafanyika ikiwa ni siku moja kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kufanya ziara ya kiserikali jijini hapa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Jiji la Mwanza, Christopher Wambura, alisema mgomo huo umesababishwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hassan Hida, kugoma kukutana nao ili kujadili malalamiko yao.

“Sababu kuu iliyosababisha wafanyabiashara wagome ni ada ya leseni ambazo hazina kiwango maalumu.

“Tumelalamika sana juu ya jambo hili, lakini mkurugenzi wa jiji amegoma kukutana na sisi, kwa hiyo ili kuonyesha kwamba hatutaki kunyanyaswa, tumeona tuitishe mgomo wa bila kikomo.

“Yaani mtu mwingine anatozwa shilingi 100,000, mwingine shilingi 150,000 hadi 300,000, sasa huu ni utaratibu gani?” alihoji Wambura.

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliozungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, waliiomba Serikali kufanya mazungumzo ya kina na wafanyabiashara hao ili kutafuta ufumbuzi wa madai yao.

Akizungumzia mgomo huo, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliutaka uongozi wa jiji hilo kutopuuza malalamiko ya wafanyabiashara hao.

Alisema yeye yuko pamoja na wafanyabiashara kwa sababu anaamini wana hoja za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Hida alisema hatua ya JWT kuhamasisha mgomo kwa madai ya kutosikilizwa na uongozi wa jiji siyo ya kweli na kwamba mgomo huo ni batili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles