24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara 20 mbaroni kwa kununua korosho kwa bei chee

Aziza Masoud-Dar es Salaam



WAFANYABIASHARA 20 wamefikisha mahakamani kwa tuhuma za kununua korosho kwa bei ya chini ya Sh 1,600 kutoka kwa wakulima na kuiuzia serikali kwa Sh 3,300.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji, Joseph Kakunda

baada ya kutembelea mabanda ya kampuni mbalimbali zilizoshirikishi maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade),

“Hawa ni wale ambao walikuwa wanajifanya wakulima kumbe  hawakuwa wakulima halisi, yaani wao walinunua korosho kwa bei ya chini kutoka kwa watu shambani wakazileta kuuza kwa serikali.

“Wale tunawahesabu kama waliwazulumu wakulima tunaendelea kuwashughulikia wapo waliopelekwa mahakamani na bado wanaendelea kupelekwa,”alisema Kakunda.

Katika hatua nyingine alisema Serikali inatarajia kukusanya tani 70,000  za korosho katika kipindi cha mwezi Desemba  kutoka kwa wakulima wa zao hilo waliopo katika mikoa ya Kusini.

Alisema  tani hizo ni kati ya 275,0000  zinazorajiwa kukusanywa katika msimu mzima.

“Mpaka juzi tumeshakusanya korosho zaidi ya tani 100,000 ambazo tumewalipa wakulima Sh bilioni 40, kwa mwezi Desemba tunatarajia kukusanya tani 70,000 kutoka kwa wakulima,”alisema Kakunda.

Akizungumzia kuhusu maonesho hayo ya siku tano ambayo yameanza jana  na yanatajiwa kumalizika Desemba 9 Kakunda alisema jumla ya washiriki 513 ukilinganisha na 506 wa mwaka jana  ambao ni  taasisi za fedha na serikali  pamoja na wenye viwanda vidogo,vya  kati na vikubwa  wanatarajia kushiriki.

Alisema katika maonesho hayo kipaumbele   ni viwanda vyenye thamani ya mazao ili kusaidia wakulima kuuza mazoa ghafi.

Aliongeza  kipaumbele kingine ni kuwa na viwanda vya kutengeneza bidhaa zinazotegemewa na watanzania pamoja na kujenga viwanda vinavyotoa ajira nyingi hasa kwa wanawake.

Kwa upande wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda(UNIDO) Stephen Kargbo alisema shirika hilo limefurahi kuwa miongoni mwa wadhamini wa maonesho hayo ambayo ni muhimu katika sekta ya viwanda nchini.

“Tunafuraha kuwa sehemu ya maonyrsho haya kwa mwaka hu,kama utamaduni wetu ulivyo tunatumia ghafla kama hizi kueleza umuhimu wa sekta ya viwanda kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania na  Afrika kwa ujumla,”alisema.

Maonyesho hayo ambayo kauli mbiyu yake ni ‘Tanzania ya sasa tunajenga viwanda’ yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba)  yanatarajiwa kufunguliwa rasmi leo na kufungwa Desemba 9.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles