24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

WAENDESHA BODABODA WAGOMA

Na  Walter    Mguluchuma-Katavi

WAMILIKI  na madreva  wa   bajaji wanaofanya   shughuli za  usafiri  katika  Manispaa ya   Mpanda  mkoani  Katavi,wamefanya   mgomo na  kusitisha  kutoa  huduma  za  usafiri   katika  maeneo ya   Manispaa ya  Mpanda  na   nje  ya    Manispaa baada  ya  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi na Majini ( SUMATRA),  kupiga  marufuku  bajaji  kufanya   safari zake kupitia   barabara kuu.

Mwenyekiti wa   wa    madreva  wa    Bajaji, Rashid   Juma   alisema  wameamua  kusitisha  kutoa  huduma  ya  usafiri  kwenye  maeneo  ya  Manispaa ya   Mpanda, baada ya  SUMATRA  kupiga  marufuku   bajaji  zote ili kupunguza wingi wa ajali.

Alisema wameamua  kusitisha  huduma  hiyo kuanzia juzi, ingawa walikuwa wamepata agizo, bali   wamesitisha  kutoa  huduma  kwenye    maeneo  yote  hata  yale  ya  barabara  ndogo.

Alisema kitendo cha  kuwazuia, kitawafanya wakose  mapato  na  kusabisha   kushindwa  kulipa kodi kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mwenyekiti wa  wasafirishaji  ambaye  pia  ni  Mwenyekiti wa    Kamati ya Usalama  Barabarani wa  Mkoa wa   Katavi, Nassor   Arfi  alisema  amepata taarifa  za   kusimamishwa  huduma   za usafiri  wa    bajaji kupita  kwenye   barabara kuu  za   Mpanda-  Kigoma,Mpanda  Sumbawanga   na   Mpanda – Tabora  na   amefanya  mawasiliano na   Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi, Meja Jenerali Raphael Muhuga.

Alisema mkoa huo, hauna nyingine    mbadala   za kuwafanya   madreva wa  majaji   kutumia,  hivyo ni   vema   mamlaka hiyo ikatumia   busara kumaliza suala hilo.

Meneja  wa  SUMATRA  wa   Mkoa  wa   Katavi, Amani  Mwakalebela  alisema mambo yote yanaendeshwa  kwa sheria halali.

Mkazi  wa Mtaa wa Kazima, Aglipina Petro  alisema    ameshindwa kumpeleka   mgonjwa  wake  hospitali,  baada  ya  kukosa  huduma  ya  usafiri.

Mkazi wa Kijiji cha Ibindi, Joice  Longino  alisema kitendo  cha    bajaji  kusitisha  huduma ya  usafiri  kumesababisha   wafanyabiashara   kushindwa   kufika  mjini   Mpanda  kununua  bidhaa kwa   ajiri ya  biashara  zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles