24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wadhamini waendelea kuwasotesha rumande Amber Rutty, mpenzi wake

Na KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

Mcheza video, Rutyfiya Abubakary maarufu kwa jina la Amber Rutty na mpenzi wake, Said Bakary Mtopali wanaoshtakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanaendelea kusota rumande kwa kukosa wadhamini.

Washtakiwa hao na mwenzao, James Delicious aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana walipanda kizimbani jana kwa mara ya pili wakati kesi yao hiyo ikitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Novemba 2 mwaka huu lakini Amber Ruty na Said Bakary Mtopali walishindwa kutimiza masharti ya dhamana kama walivyoshindwa tena leo Novemba 12 na hivyo kupelekwa gerezani.

Awali Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai kuwa kosa la kwanza linalomkabili Amber Rutty ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile kosa linalodaiwa kutendwa kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu, Said Bakary Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile.

Shtaka lingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili mshtakiwa wa pili, Said Bakary Mtopali ambapo anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 jijini Dar es Salaam mtuhumiwa alifanya mapenzi na Amber Ruty kinyume na maumbile.

Kosa la tatu ni kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious anayedaiwa kati ya Oktoba 25, 2018 amesambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine linalowakabili watuhumiwa hao Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono kosa ambalo wanadaiwa kulitenda Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha hizo kupitia makundi ya Whatsapp.

Washtakiwa walipewa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 kila mmoja na kusaini dhamana ya maandishi ya Sh Milioni 15.

Pia wadhamini wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati z za kusafiria na wasitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles