24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WADAU WAIPONGEZA SERIKALI KUONDOA VAT KWENYE TAULO ZA KIKE

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wa bidhaa za taulo za kike, (pedi), wameipongeza hatua ya serikali kupunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT),  kwa bidhaa hiyo kwa asilimia 18.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Julai 11, wadau hao wamesema kitendo cha kushuka kwa kodi hiyo kimewafanya wapunguze bei ya taulo hizo.

“Baada ya kusikia serikali imepunguza kodi ya VAT kwa asilimia 18, tumeamua kupunguza bei ya bidhaa za taulo ya kike kwa gharama ya Sh 59,000 kutoka Sh 65000 Kwa bei ya jumla,” amesema Meneja Mkuu wa Kampuni ya NN General Supplies Vumilia Tomito inayosambaza pedi aina ya HC.

Aidha, amesema kutokana na hali hiyo, bei ya reja reja ya bidhaa hiyo itakua Sh 2,800 kutoka Sh 3,500 kwenye maduka mbalimbali nchini.

“Kwa sasa kampuni yetu iko kwenye mchakato wa ujenzi wa kiwanda cha pedi mara baada ya kukamilika kwa mazungunzo na serikali,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles