23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wahofia misitu ya asili kutoweka baada ya miaka 40

Victor Makinda, Mororgoro

MKURUGENZI wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Charles Meshack, amesema kutokana na Serikali kuruhusu misitu ya vijiji kutumika kama mashamba, kunasababisha ekari 469,000 za misitu kupotea kila mwaka na hatua zisipochukuliwa ndani ya miaka 40 itatoweka yote.

Alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 19 wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (MJUMITA) na kwamba misitu ya asili bado haina thamani mbele ya kilimo.

Alisema ipo haja ya wadau wa misitu kuendelea kuonesha thamani ya mazao ya misitu kwa jamii na kufanya wasimamizi ikiwemo vijiji kunufaika na kuachana na dhana ya kutegemea kilimo kama chanzo pekee cha uchumi.

Aidha alisema nguvu za wadau katika  usimamizi shirikishi na uhifadhi wa misitu  zimeendelea kuonekana licha ya Serikali kuwa na uwekezaji mdogo katika usimamizi huo.

Meshack alisema wakati umefika mfumo wa usimamizi wa  misitu unaotekelezwa na MJUMITA kuendelezwa nchi nzima ili kutetea misitu ya asili  ambapo hekali milioni 96 iliyobaki  huenda ikapotea ndani ya miaka 40 ijayo kama maeneo mengi ya misitu yakiendelea kufyekwa na kutumika kama mashamba na  malisho ya mifugo.

Aliishauri MJUMITA kuendelea kisimamia misitu hiyo ili kumilikiwa na wananchi wenyewe na kuendelea kunufaisha jamii.

Awali Ofisa Misitu Mkoa wa Morogoro, Josephat Chuwa, alisema misitu iliyopo haijapewa thamani inayolingana nayo.

Alitolea mfano misitu ya hifadhi ya Tao la Mashariki ambayo imekuwa ikichukua nafasi kubwa katika kuinua uchumi wa nchi kwa sababu asilimia 25 ya Watanzania wanatumia maji yanayotokana na vyanzo vilivyopo katika misitu iliyopo tao ya la mashariki  na asilimia 60 ya nishati ya umeme unatokana na vyanzo misitu hiyo ya tao la mashariki.

Chua alisema asilimia 75 ya maji yanayotumika  jijini Dar es salaam yanatokana na vyanzo vilivyo katika milima hiyo ya tao la mashariki.

Alisema ni vema jamii ikafahamu umuhimu wa utunzaji wa misitu na kuona kwamba hakuna misitu hakuna huduma hizo muhimu kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles