26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WACHOCHEZI KWENYE WHATSAPP KUBANWA

Na AZIZA MASOUD- DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi limewataka viongozi wa makundi ya mitandao ya kijamii hasa WhatsApp, kuwajibika kwa kutoa taarifa  za watu wanaofanya makosa ya kimtandao kwa kutuma taarifa za  kichochezi na udhalilishaji ili waweze kuchukuliwa hatua.

Tahadhari hiyo imetolewa kwa viongozi wa makundi hayo jana na Mratibu Msaidizi wa Polisi na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Uhalifu Mtandaoni  Makao Makuu ya jeshi hilo, Joshua Mwangasa, katika semina ya viongozi wa dini iliyolenga kuhamasisha matumizi bora ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Alisema katika makundi ya Whats App kumekuwa kukifanyika makosa mengi ya kimtandao kwa kuwa watumiaji wanahisi   maeneo hayo ni sehemu salama  ya kujificha na mkono wa dola.

“Maadmin (viongozi) waliopo katika makundi nao hawajui wajibu wao, wanapaswa kufahamu kuwa wanapaswa  kumripoti polisi kwa mtu yeyote anayetuma ujumbe wa kichochezi kama kudhalilisha kwa kuwa wasipofanya hivyo ikitokea tumejua lazima wao ndio watakuwa wa kwanza kuulizwa,” alisema Mwangasa.

Alisema makundi mengi ya WhatsApp yanaendeshwa kinyume na dhamira iliyowekwa na kusababisha watu kujadili ama kuleta taarifa tofauti na malengo ya kundi husika.

“Madmin (viongozi wa makundi) tuhakikishe group (kundi) zinafanya kazi iliyokusudiwa, wewe admini ukikaa kimya baadaye polisi wakisikia kuna tatizo ndani ya group lako lazima utahitajika kutoa ushirikiano,” alisema Mwangasa.

Akizungumzia idadi ya makosa ya kimtandao, alisema imeongezeka kutoka  5,172 mwaka 2015 hadi 9,441 mwaka jana ambayo ni sawa na ongezeko la mashauri 4,269.

Alisema kwa mwaka huu jumla ya kesi  3,346 zimeripotiwa katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni na baadhi tayari zimeshafikishwa mahakamani.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, alisema matumizi ya simu za mkononi kwa sasa yamekuwa kama silaha na endapo zitatumika vibaya zinaweza kusababisha madhara makubwa.

“Simu za mkononi kwa sasa zimekuwa kama silaha, lugha na maudhui unayotumia unapaswa kuyafikiria kabla ya kutuma sehemu yoyote,” alisema Mhandisi Kilaba.

Alisema TCRA itaendelea kuhakikisha teknolojia ya mawasiliano inatumika ndani ya nchi bila kuleta madhara katika jamii.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ambaye pia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema  matumizi ya mitandao ya kijamii hasa kupitia simu za mkononi yamechangia mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles