31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wabuni mbinu mpya kupambana na Covid-19

Mary Mwita  -Arusha

KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukabiliana na Ugonjwa wa Covid-19, Shirika lisilo la Kiserikali la Convoy of Hope International Tanzania, limetoa mafunzo kwa walezi wa vituo vya watoto yatima jijini Arusha na kuwafundisha mbinu mpya na rahisi ya kutumia Kibuyu Chirizi kunawia mikono.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Convoy of Hope International Tanzania, Geofrey Mjema alisema Shirika hilo linajali afya za watu wanaowahudumia ikiwa ni pamoja na watoto.

Mjema alisema kuwa ugonjwa wa Covid-19 unatishia maisha ya watu na kuwa Shirika la Convoy likiwa shirika la dini litambua umuhimu wa kujitoa kwa hali na mali katika kusaidia watu ikiwa ni msingi wa imani na upendo imani yao .

Alisema Shirika hilo limedhamiria kuungana na Serikali katika kampeni ya kukabiliana na mapambano ya ugonjwa wa Covid-19 na kudai kuwa wanatoa elimu sehemu za vijijini na pia katika makanisa wanayohudumia.

Akitoa ufafanuzi wa matumizi ya Kibuyu Chirizi kwa wamiliki na walezi  wa vituo vya watoto  yatima, ofisa kutoka shirika hilo, Winfrida Roman, alisema matumizi ya njia hiyo ni rahisi kwa kuwa ina gharama rahisi na inatumia dumu la lita tano, vijiti vinne, kamba na na msumari wa kutobolea dumu kwa ajili ya kuwekea maji.

Roman alisema kuwa vibuyu chirizi havina gharama na kuwa wamiliki wa vituo wanaweza kutengeneza kwa wingi bila gharama kubwa kama ilivyo vifaa vingine.

Roman alisema kuwa Convoy of Hope International Tanzania wana miradi ya lishe katika shule zilizo vijijini na kuwa mbinu hiyo walianza kuitumia muda mrefu na kuwa wanaendelea kutoa elimu hiyo ili kuepusha maambukizi ya Covid-19

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles