27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE WAVUTANA MUSWADA WA DODOMA KUWA MAKAO MAKUU

Mwandishi Wetu, Dodoma


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mara ya kwanza kimewasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge kuhusu muswada wa kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi huku wakivutana na Spika Job Ndugai, kuhusu maana ya maneno ‘City na Capital City’.

Akiwasilisha maoni hayo, Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda (Chadema), alianza kwa kusema serikali viongozi wa serikali wamekuwa wakinunua wabunge wa upinzani jambo lililopingwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambapo alitoa taarifa kwa kumtaka Mwakagenda kuacha kutuhumu viongozi wa serikali.

“Mheshimiwa Spika, kanuni zinakataza kutojadili suala ambalo halipo mezani na limekwishatolewa ufafanuzi lakini pia amekuwa akituhumu viongozi wa serikali kuwa wananunua wabunge, lakini tangu chaguzi zimeanza si yeye wala yeyote aliyeshtaki popote, jambo hili ni uongo na kuwa serikaki ilipotamka Dodoma kuwa Jiji ilivunja sheria, tunazungumzia makao makuu si jiji,” amesema Jenista.

Wakati Jenista akiendelea alimtaka Mwakagenda kuondoa baadhi ya maneno  katika hotuba hiyo jambo lililopingwa na Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), ambaye alisema asiichambue hotuba hiyo kwani hawajaisikiliza.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisema walicholetewa ili kujadili ni ‘declaration of Capital City’ hvyo Mwakagenda yuko sahihi, kauli hiyo ilipingwa na Spika Ndugai ambapo alimtaka kuelewa maana ya City na Capital City ni vitu viwili tofau yaani Jiji na Makao Makuu.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimwambia Mwakagenda amesikia alivyoambiwa na kumuuliza anasemaje ambapo alijibu hiyo ni hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na si ya CCM ambapo aliendelea kusoma akitaja Dodoma kuwa jiji badala ya makao makuu na kuhusu CCM inavyonunua wapinzani.

“Mheshimiwa Mwakagenda, kilichopo mezani ni muswada si nani kanunuliwa, tukienda kwenye kamati ya maadili uthibitishe, wewe soma tu mambo ya uchaguzi lakini ukimaliza tutakupeleka kwa wenzako (Kamati ya Maadili),” amesema Spika.

Aidha, alisimama tena na kusema: “Mheshimiwa Spika huo ulikuwa ni utangulizi wangu tu kama wengine wanavyompongeza Chiza, na haya ndiyo madhara ya kutuondolea wataalamu wa kutuandikia hotuba, hii tumeiandaa wenyewe.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles