24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge, wanajeshi walia njaa Uganda

KAMPALA, UGANDA

WABUNGE, maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) na wengine wa Serikali wanalalamika kichinichini kutolipwa mishahara yao, gazeti la Daily Monitor la hapa limefichua.

Daily Monitor limeripoti kuwa wabunge na maofisa hao wengine wamekosa mshahara kwa miezi miwili mfululizo.

Wabunge watatu waliozungumza kwa masharti ya kutotajwa, walithibitisha kwa gazeti hilo kuwa wamekuwa wakisubiri malipo yao bila mafanikio.

“Malipo yote yamesimamishwa kwa sasa na kila mmoja anashangaa nini kinatokea,” alisema mmoja wa wabunge hao.

Malipo yaliyoathirika ni pamoja na fedha kwa ajili ya kusafiria ndani ya nchi ikiwamo majimboni na usimamiaji wa huduma zinazotolewa na Serikali, posho za kusafiri ng’ambo na za vikao.

Kila mbunge anastahili Sh 50,000 za Uganda (Sh 30,000 za Tanzania) kwa kila anapohudhuria kikao cha Kamati ya Bunge na Sh 100,000 (Tsh 60,000) anapohudhuria kikao cha Bunge.

Mbunge mwingine alisema: “Wanasema si sisi tu tulioathirika. UPDF na mashirika mengine ya Serikali yanakabiliwa na tatizo hili, hakuna fedha.”

Alisema tatizo hilo lilisababisha kusimama kwa mipango ya awali ya kuanza shughuli za wilaya mpya na vitengo vyake.

Aidha alisema pia lilisababisha kusitishwa kwa usimikaji wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa na Rais Juni mwaka huu.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha Matia Kasaijan alipotakiwa ufafanuzi na gazeti hilo alisema; “Spika ameniambia kitu kama hicho, lakini bado sijafuatilia, ninahitaji kuchunguza na kukupatia taarifa baadaye.”

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masuala ya Umma wa Bunge, Chris Obore alisema; “Tunaomba uvumilivu zaidi, wabunge, watapata malipo yao. Si rahisi kuongeza bajeti yako iwapo ilipunguzwa kwa Sh bilioni 100.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles