29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE WA UPINZANI WASUSIA BUNGE KUPINGA KUKAMTWA KWA LISSU

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) akiongoza wapinzani kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Wabunge wa upinzani watoka nje ya Bunge kupinga kukamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)  Tundu Lissu.

Wabunge hao wametoka nje ya Bunge hivi punde baada ya Naibu Spika kumtaka Mbunge wa Serengeti kutoka nje baada ya kutokea mabishano yaliyotokana na hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) ya kutaka Bunge lijadili swala Haki na Madaraka ya Bunge kukiukwa kwa wabunge kukamatwa ndani ya viwanja vya Bunge kinyume na utaratibu.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amewatoa nje ya Bunge, wabunge watatu wa CHADEMA, Halima Mdee (Kawe), Esther Bulaya (Bunda) na Marwa Ryoba (Serengeti).

Pamoja na hilo, baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi, Tundu Lissu amerejeshwa mahabusu hadi kesho ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles