25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wa upinzani wamvaa Dk. Mwakyembe

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe.

Na MAREGESI PAUL, DODOMA

BAADHI ya wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wamemshambulia Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe wakisema Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa wa Mwaka 2016 aliouwasilisha bungeni juzi, unataka kuviua vyombo vya habari nchini.

Walisema hawako tayari kuuunga mkono kwa kuwa umewasilishwa kwa nia ovu ambayo hawawezi kuikubali kwa namna yoyote.

Wabunge hao waliyasema hayo bungeni juzi na jana walipokuwa wakichangia muswada huo kwa nyakati tofauti baada ya kusomwa kwa mara ya pili juzi na Dk.  Mwakyembe.

Aliyekuwa wa kwanza kumshambulia Dk.Mwakyembe ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ambaye alisema pamoja na ubovu wa muswada huo, lazima utapitishwa na wabunge wa CCM kwa kuwa ni wengi bungeni.

“Huu muswada ni mbovu kabisa na namshangaa Dk. Mwakyembe pamoja na usomi wake, anakubali kuleta kitu anachojua kinalenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

“Dk. Mwakyembe huyu huyu ndiye aliyetetea kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia mikutano ya hadhara wakati akijua inaruhusiwa katika katiba.

“Katika nchi hii sheria mbovu zinaletwa lakini kwa wingi wenu mnapitisha tu ila mjue mshahara wa dhambi ni mauti,” alisema Lema.

Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alisema anashindwa kuelewa nia ya Dk. Mwakyembe ya kuwasilisha muswada huo wakati akijua unalenga kuua vyombo vya habari nchini.

“Napata ukakasi juu ya Dk. Mwakyembe kuleta muswada huu, yaani sielewi Serikali ina nia gani na vyombo vya habari nchini.

“Katika nchi hii, hivi sasa kila mtu ni muoga, mtu mmoja anavunja Katiba watu hawasemi, wanaogopa hata kumshauri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles